Church Missionary Society (CMS)
Church Missionary Society (CMS) (Shirika la kimisionari la kanisa) ni shirika la umisionari la Kanisa Anglikana lililoanzishwa mwaka 1799 huko London (Uingereza).
Mianzo ya CMS
[hariri | hariri chanzo]CMS haikuwa shirika la kwanza ya misioni katika Kanisa Anglikana. Lilitokea katika harakati ya kiinjili yaani maungano ya Wakristo (si chombo cha uongozi wa kanisa) waliotaka kuchangia katika ujenzi wa kanisa kwa hiari yao. Walikazia imani kufuatana na jinsi walivyoelewa Biblia, kupokea imani kwa moyo na maisha kulingana na maadili ya imani.
Kazi katika Freetown
[hariri | hariri chanzo]CMS ilianzishwa mwaka 1799 kwa jina la "Shirika la misioni kwa Afrika na Mashariki" (Society for Missions in Africa and the East) Ilikuwa na mwanzo mgumu kwa sababu katika miaka kumi ya kwanza ilikosa kabisa Waingereza waliojitolea kupokea wito la kwenda Afrika. Kwa hiyo CMS ilianza na Wajerumani Walutheri wawili Melchior Renner kutoka Wurtemberg na Peter Hartwig kutoka Prussia waliokubali kwenda 31 Januari 1804 kwenda Freetown (Sierra Leone) na kuanza kazi na watoto Waafrika waliokombolewa kutoka utumwani.
Hadi mwaka 1813 CMS ilituma Freetown wamisionari 8 -wote Wajerumani Walutheri- pamoja na wakristo raia kama wakulima na walimu ikatunza watoto 120 walionunuliwa kutoka utumwani au kuokelewa na jeshi la Uingereza kutoka jahazi za wafanyabiashara ya watuma.
Shirika la kikanisa
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1812 Shirika lilibadilisha jina kuwa "The Church Missionary Society for Africa and the East". Liliendelea kupanusha maeneo yake ya kazi hadi Uhindi na New Zealand.
Mwaka 1841 shirika lilijiweka kabisa chini ya maaskofu wa Kanisa Anglikana.
CMS katika Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]1837 shirika lilianza kazi katika Ethiopia kwa matumaini kuchangia katika maendeleo ya kanisa la liorthodoksi na kuhubiri injili kati ya makabila ya Wagalla katika kusini ya nchi. Lakini wasiwasi kati ya viongozi wa Ethiopia kuhusu kuongezeka kwa wageni nchini ziliwapasa Waprotestant kuondoka 1842.
Uswahilini
[hariri | hariri chanzo]Mmoja kati ya wamisionari kutoka Ethiopia Mjerumani Dr. Ludwig Krapf aliamua kuwalenga Wagalla kutoka pwani la Afrika ya Mashariki. 1844 alifika Zanziibar akajipatia kibali cha Sultani Sayyid Said cha kuanzisha kituo cha misioni huko Mombasa. 1844 Krapf alifika Mombasa akianza mara moja kujifunza Kiswahili pamoja na lugha ya Mijikenda walio wazalendo wa eneo hili. Hapa Mombasa mke na mtoto waliugua Malaria wakafa. Krapf akahamia ndani ya bara akaanzisha kituo cha Rabai Mpya. 1846 misionari mwingine Johannes Rebmann alikuja na kufanya kazi pamoja naye. Hapa Rabai Mpya Krapf alitunga kamusi na sarufi ya Kiswahili ya kwanza. Krapf hakufaulu kuwafikia Wagalla wala kuwabatiza watu wengi tena lakini aliweka msingi muhimu kwa maendeleo ya kanisa la kikristo pia kwa jamii yote ya Afrika ya Mashariki kwa kazi yake ya kilugha.
Kwa ujumla CMS ilianzisha kanisa la kikristo mahali pengi duniani. Katika Afrika ya Magharibi iliwahi kuwabariki Waafrika kuwa mapadre na 1864 huko Nigeria Samuel Ajayi Crowther alibarikiwa kuwa askofu wa kwanza Mwafrika katika Kanisa Anglikana pia katika makanisa ya kiprotestant yote.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Taarifa juu ya wamisionari wa kwanza wa CMS Ilihifadhiwa 30 Agosti 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Church Missionary Society (CMS) kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |