Content-Length: 126096 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/World_Trade_Organization

Shirika la Biashara Duniani - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Shirika la Biashara Duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka World Trade Organization)
Nchi wanachama wa WTO;
Kijani cheusi: nchi zilizoanzisha WTO mwaka 1995;
Kijani cheupe: nchi zilizojiunga baadaye

Shirika la Biashara Duniani (kifupi: WTO; Kiing. World Trade Organization, WTO; Kifar. Organisation Mondiale du Commerce, OMC; Kihisp. Organización Mundial de Comercio, OMC) ni shirika la kimataifa linaloshughulika utaratibu wa biashara duniani. Shabaha ya kazi yake ni kuondoa kwa vizuizi ya biashara kati ya mataifa. Makao makuu yake yapo Geneva (Uswisi).

WTO ina nchi wanachama 153. Ilianzishwa tar. 1 Januari 1995 ikitanguliwa na Mkataba wa Kimataifa juu ya Forodha na Biashara (GATT, General Agreement on Tariffs and Trade). Pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia iko taasisi muhimu inayoangalia uchumi na biashara ya duina yote.

Katiba ya WTO inataja kama shabaha yake kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na biashara ili kuinua kiwango cha maisha, kuhakikisha watu wengi wanapata ajira, kuhakikisha mapato na mahitaji halisi yanaongezeka; kutumia ipasavyo maliasili duniani, kupanua uzalishaji wa bidhaa na kazi ya huduma; kufikia makubaliano ya kunufaishana; kupunguza kwa kiasi kikubwa na kufuta ushuru forodha na kuondoa vikwazo vingine vya kibiashara.









ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/World_Trade_Organization

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy