Content-Length: 257527 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Azerbaijan

Azerbaijan - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Azerbaijan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Azərbaycan Respublikası
Jamhuri ya Azerbaijan
Bendera ya Azerbaijan Nembo ya Azerbaijan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Azərbaycan Respublikasının Dövlət Himni
Lokeshen ya Azerbaijan
Mji mkuu Baku
40°22′ N 49°53′ E
Mji mkubwa nchini Baku
Lugha rasmi Kiazeri
Serikali Jamhuri
Ilham Aliyev (İlham Əliyev)
Ali Asadov (Əli Əsədov)
Uhuru
Ilitangazwa
Ilikamilishwa

30 Agosti 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
86,600 km² (ya 112)
1.6
Idadi ya watu
 - 2019 kadirio
 - 1999 sensa
 - Msongamano wa watu
 
10,097,171[1] (ya 91)
7,953,438
115/km² (ya 99)
Fedha Manat (AZN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+4)
(UTC+5)
Intaneti TLD .az
Kodi ya simu +994

-


Ramani ya Azerbaijan

Azerbaijan (pia: Azabajani, Azebajani) ni nchi ya Kaukazi kati ya Ulaya na Asia.

Imepakana na bahari ya Kaspi, Urusi, Georgia, Uturuki, Armenia na Uajemi.

Azerbaijan ni pia jina la mikoa miwili magharibi mwa Uajemi (Azerbaijan ya Mashariki na Azerbaijan ya Magharibi); nchini Uajemi takriban 16% za wakazi ni Waazeri; kwa jumla walioko Uajemi ni wengi kushinda walioko Azerbaijan yenyewe.

Eneo la Nakhichevan ni sehemu ya Azerbaijan inayopakana na Uturuki na Uajemi lakini imetenganika na sehemu kubwa ya nchi kwa sababu katikati kuna eneo la Armenia.

Eneo la Nagorno-Karabakh linalokaliwa na Waarmenia ndani ya Azerbaijan lilijitangaza nchi huru mwaka 1991 lakini haijatambuliwa na umma wa kimataifa.

Azerbaijan ni nchi mwanachama wa baraza la Ulaya tangu mwaka 2001. Hivyo kisiasa inahesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya, lakini kijiografia mara nyingi yahesabiwa kuwa sehemu ya Asia ya Magharibi.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Mlima mkubwa ni Bazardüzü kwenye Kaukazi wenye kimo cha mita 4.466.

Ziwa kubwa ni Sarisu lenye eneo la km² 67.

Mto Kura unapita eneo la nchi na kuishia katika Bahari ya Kaspi baada ya mwendo wa km 1,515.

Azerbaijan ina visiwa viwili vya Pirallahı na Cilov kwenye Bahari ya Kaspi.

Kwenye rasi ya Abşeron kuna mafuta ya petroli.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Azerbaijan ina historia ndefu kuanzia Zama za Mawe.

Kuanzia karne ya 9 KK ilikaliwa na Washitia, halafu Wamedi, wote wa jamii ya Waajemi ambao walishinda na kuunda dola kubwa kati ya karne ya 6 KK. Tangu hapo Uzoroastro ulienea nchini.

Baadaye eneo hilo liliingizwa katika Ugiriki wa Kale chini ya Aleksanda Mkuu hadi karne ya 4 KK wakazi wa Kaukazi walianzisha ufalme wa kwao ambao katika karne ya 4 BK ulipokea Ukristo kama dini rasmi.

Kwa kuwa ufalme huo kuanzia mwaka 252 ulikuwa chini ya himaya ya Dola la Wasasanidi wa Uajemi, hao waliposhindwa na Waarabu Waislamu, Azerbaijan iliingia bila kutaka katika mtandao wao (667).

Kuanzia mwaka 1067 watu wa jamii ya Waturuki walianza kuenea nchini pamoja na lugha yao.

Mwanzoni mwa karne ya 19 Urusi iliteka eneo hilo kutoka kwa Waajemi.

Jaribio la Kaukazi Kusini kujitenga baada ya vita vikuu vya kwanza lilishindikana mwaka 1918. Vilevile jaribio kama hilo la Azerbaijan peke yake lilikomeshwa mwaka 1920.

Hatimaye uhuru ulipatikana mwaka 1991, kwa Umoja wa Kisovyeti kusambaratika.

Azerbaijan siku hizi inakaliwa hasa na Waazeri (91.6%) wanaoongea Kiazeri ambacho ni karibu sana na Kituruki. Ndicho lugha rasmi.

Lugha nyingine zinazotumika sana katika elimu na mawasiliano ni Kirusi na Kiingereza.

Wakazi wengi (97%) ni Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia (85%). Lakini nchi haina dini rasmi, pia kwa sababu kwa wengi suala la dini si muhimu kimaisha.

Wakristo ni 3.1%, wakiwemo hasa Waorthodoksi (Warusi na Wageorgia) na Waorthodoksi wa Mashariki (Kanisa la Kitume la Armenia).

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. azadlıq saytı: demoqrafik vəziyyət – xəbərin yayınlanma tarixi: 11 iyun 2019

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Taarifa za jumla
Serikali
Vyombo vya habari
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Azerbaijan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Azerbaijan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Azerbaijan

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy