Content-Length: 94194 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Herodia

Herodia - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Herodia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Herodia kadiri ya Paul Delaroche.
Sikukuu ya Herode kadiri ya Lucas Cranach the Elder, 1531.
Sikukuu ya Herode kadiri ya Peter Paul Rubens.
Salome akimkabidhi mamaye kichwa cha Yohane Mbatizaji kadiri ya Juan de Flandes, 1496.

Herodia (kwa Kigiriki Ηρωδιάς, Hērōdiás; (15 KK hivi — baada ya 39 BK) alikuwa mwanamke wa ukoo wa Herode huko Uyahudi chini ya himaya ya Dola la Roma.[1][2]

Ni maarufu hasa kwa kufanya mpango wa kumuua Yohane Mbatizaji hata akaufanikisha.

Uhusiano wa kifamilia

[hariri | hariri chanzo]

Herode Mkuu alipoua wanae Aleksanda na Aristobulo IV mwaka 7 KK, Herodia alibaki yatima, hivyo Herode alimuoza kwa mwanae Herode II.

Baadaye Herodia alitengana na mumewe ili aolewe na Herode Antipa, mtawala wa Galilaya na Perea.[5]

Herode II na Herodias walimzaa Salome (binti Herode).[6][7]

Kadiri ya Injili, Yohane Mbatizaji alifungwa na Herode Antipa kwa sababu ya kulaumu ndoa hiyo; hatimaye Herodia alifanya njama na binti yake Salome, akafaulu kumfanya Herode amkate kichwa Yohane.

Hatimaye Herode Antipa alinyang'anywa madaraka na kupelekwa uhamishoni sehemu za Ufaransa wa leo, ambako Herodia alimfuata.

  1. Herodian Dynasty
  2. http://www.perseus.tufts.edu/hopper/text?doc=Perseus%3Atext%3A1999.01.0239%3Abook%3D16%3Achapter%3D2%3Asection%3D34
  3. Harold Hoehner, Herod Antipas: A Contemporary of Jesus Christ (Zondervan, 1983), page 132 - 134.
  4. see also, for example, E. Mary Smallwood, "Behind the New Testament", Greece & Rome, Second Series, Vol. 17, No. 1 (Apr., 1970), pp. 81-99
  5. According to the historian Josephus: Herodias took upon her to confound the laws of our country, and divorced herself from her husband while he was alive, and was married to Herod Antipas
  6. Taylor, V. (1966). The gospel according to St Mark, 2nd Edition. London: Macmillan (pp310ff.)
  7. As Josephus reports in Jewish Antiquities (Book XVIII, Chapter 5, 4):

    Herodias, [...], was married to Herod, the son of Herod the Great by Mariamne II, the daughter of Simon the High Priest. [Herod II and Herodias] had a daughter, Salome...

  • Gillman, Florence Morgan. Herodias: At Home in the Fox's Den. Interfaces. Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 2003.
  • Meier, John P. A Marginal Jew: Rethinking the Historical Jesus, Volume Two: Mentor, Message and Miracles. Anchor Bible Reference Library, New York: Doubleday, 1994.
  • Theissen, Gerd. The Shadow of the Galilean: The Quest of the Historical Jesus in Narrative Form. Philadelphia: Fortress, 1987.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Herodia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Herodia

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy