Punjab
Punjab (pia: Panjab; kwa Kipunjabi: ਪੰਜਾਬ panjāb, maji tano au nchi ya mito mitano) ilikuwa jimbo la Uhindi wa Kiingereza lililogawiwa tangu 1947 kati ya nchi za Uhindi na Pakistan.
Kijiografia ni tambarare ya mito mitano inayoingia katika mto Indus upande wa mashariki. Hali ya hewa ni yabisi lakini maji ya mito ni msingi wa kilimo cha umwagiliaji. Kilimo hicho chazalisha sehemu kubwa ya chakula cha Uhindi na Pakistan.
Panjab ni chanzo cha ustaarabu wa Uhindi wa Kale na maghofu ya Harappa yako huko. Hadithi nyingi za maandiko matakatifu ya Uhindu kama Rig Veda, Upanishadi na Mahabarata yaliandikwa huko.
Asili ya dini ya Kalasinga pia iko Punjab.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Punjab kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |