Content-Length: 67512 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Voortrekker

Voortrekker - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Voortrekker

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makaburu safarini, picha mnamo 1860
Kumbukumbu ya Voortrekker mjini Pretoria

Voortrekker ni neno la Kiafrikaans linalomaanisha "watangulizi". Katika historia ya Afrika Kusini makaburu walianza kuondoka katika Koloni ya Rasi kuanzia mwaka 1835 kwa sababu walisikitika mno utawala wa Uingereza.

Chanzo cha kutoka kwa mavoortrekker

[hariri | hariri chanzo]

Hasa katika miaka ya 1840 na 1850 maelfu waliondoka katika koloni ya Kiingereza na kuingia katika maeneo ya kaskazini ya Afrika Kusini. Walisafiri hasa kwa kutumia magari yaliyovutwa na maksai pamoja na mifugo na familia yote wakiishi katika hema kwa miezi hata miaka hadi kufikia mahali walipoweza kujenga. Walianzisha jamhuri ndogo kama vile Transvaal, Dola Huru la Oranje na Natalia.

Vita na wazalendo

[hariri | hariri chanzo]

Upanuzi huu ulisababisha vita mbalimbali kati yao na makabila ya Waafrika kama Wandebele au Wazulu. Lakini maeneo makubwa ya Afrika Kusini yalikuwa karibu bila watu kutokana na vita za mfecane zilizoendeshwa na Shaka Zulu kabla ya upanuzi wa makaburu. Kwa jumla mavoortrekker waliweza kujitetea kwa sababu walikuwa na silaha bora kuliko Waafrika pia kwa sababu viongozi Waafrika walishindana kati yao na hawakusimama pamoja.

Viongozi

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya viongozi wa mavoortrekker walikuwa Piet Retief, Gerrit Maritz, Andries Pretorius, Louis Trichardt, Hendrik Potgieter na wengine.

Majina yao yapatikana katika majina ya miji ya Afrika Kusini hata kama serikali imeanza kutumia majina mapya tangu mwisho wa siasa ya Apartheid. Mifano ya majina ya Kivoortrekker ni Pretorius (mji wa Pretoria), Potgieter (Potchefstroom), Louis Trichardt (mji wa Louis Trichardt ulioitwa kwa muda Makhado), Piet Retief (mji wa Piet Retief katika jimbo la Mpumalanga)

Mwisho na kumbukumbu

[hariri | hariri chanzo]

Kwenye mwisho wa karne ya 19 jamhuri zote zilizoanzishwa na mavoortrekker zilivamiwa na kutwaliwa na Uingereza uliopanusha utawala wake juu ya Afrika Kusini yote.

Kuna kumbukumbu kubwa kwa heshima ya Voortrekker mjini Pretoria iliyojengwa wakati wa siasa ya Apartheid na leo kazi yake ni kama makumbusho ya utamaduni wa Kiafrikaans.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Voortrekker kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Voortrekker

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy