Injili ya Mathayo ni kitabu cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Ukurasa wa kwanza wa Injili ya Mathayo ulichorwa mnamo mwaka 1240 Ulaya ukionyesha mamajusi watatu mbele ya mtoto Yesu.
Mchoro huu kutoka Ufaransa (mnamo mwaka 800) wamuonyesha Mwinjili Mathayo akipokea maneno ya Injili yake kutoka kwa malaika.
Agano Jipya

Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Marko na Luka, kwa sababu inafanana nazo kwa kiasi kikubwa; hasa inatumia asilimia 80 ya maandiko ya mwinjili Marko.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi

hariri

Katika matoleo ya Biblia kichwa cha kitabu ni "Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo" lakini kichwa hiki si sehemu ya toleo asili la Kigiriki.

Ingawa Injili yenyewe haimtaji mwandishi wake, kuanzia Papias (mnamo mwaka 130) Mtume Mathayo ametajwa kama mwandishi wa misemo ya Yesu Kristo kwa lugha ya Kiebrania.

Wataalamu wanajadili kiasi gani maandishi yake yamechangia Injili hii jinsi ilivyo.

Muda wa uandishi

hariri

Wakati wa kutolewa unaaminiwa na wataalamu wengi wa kisasa ilikuwa kati ya mwaka 80 na 90, yaani baada ya hekalu la Yerusalemu kubomolewa, tena baada ya Wayahudi kuwatenga wenzao waliomuamini Yesu.

Tabia za Mathayo

hariri

Mathayo anakazia kuwa Yesu wa Nazareti ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale. Kwa sababu hiyo Mathayo anaripoti maneno ya Agano la Kale mara kwa mara ili kuthibitishwa yametimia katika maisha ya Yesu.

Tabia hii inachukuliwa kuthibitisha maelezo ya kwamba Injili hii ililenga Wakristo ambao walikuwa Wayahudi na kutumia lugha ya Kigiriki.

Mathayo anakazia pia mafundisho ya Yesu ilhali Marko anaeleza zaidi matendo yake.

Nembo ya Injili

hariri

Injili hii inaanza kwa kuorodhesha mababu wa Yesu. Kutokana na mwanzo huu, vizazi vya baadaye vilimpa Mwinjili Mathayo nembo la mwanamume au malaika akichora habari za Biblia.

Yaliyomo

hariri
  1. Uzazi na utoto wa Yesu (Mat 1-2)
    Ukoo wa Yesu, kuzaliwa kwake, kukimbilia Misri na mauaji ya watoto wa Bethlehemu
  2. Chanzo cha kazi yake huko Galilaya (Mat 3-4)
    Yohane Mbatizaji, Yesu ajaribiwa jangwani, Mitume wa kwanza
  3. Hotuba ya mlimani (Mat 5-7)
  4. Uponyaji na miujiza (Mat 8 – 9,34)
  5. Hotuba kuhusu umisionari wa wanafunzi
    Wito wa mitume 12 (10,1-4), tangazo la mateso yajayo (10,16-26), hofu ya watu na kumhofia Mungu (10,26-33)
  6. Mafundisho juu ya Yohane Mbatizaji, Wafarisayo na walimu wa sheria
  7. Hotuba ya mifano juu ya Ufalme wa Mungu (Mat 13)
    Mfano wa mpanzi (13,1-9; maelezo 13,18-23), magugu katika ngano (13,24-30; maelezo 13,36-43), mfano wa mbegu wa haradali (13,31-32), chachu (13,33-35), hazina iliyofichika (13,44), lulu (13,45-46), wavu wa samaki (13,47-52)
  8. Matendo mengine (Mat 13,53 - 17,27)
  9. Hotuba juu ya mahusiano kati ya wanafunzi (Mat 18)
  10. Safari ya kwenda Yerusalemu (Mat 19-22)
  11. Hotuba juu ya mwisho wa Yerusalemu na mwisho wa nyakati (Mat 23-25)
  12. Mateso na ufufuko wa Yesu (Mat 26-28)

Marejeo

hariri

Ufafanuzi

hariri
  • Allison, D.C. (2004). Matthew: A Shorter Commentary. T&T Clark. ISBN 978-0-567-08249-7. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Davies, William David; Allison, Dale C. (1988). A Critical and Exegetical Commentary on the Gospel According to Saint Matthew. Juz. la I: Introduction and Commentary on Matthew I–VII. T&T Clark Ltd. ISBN 9780567094810. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Davies, William David; Allison, Dale C. (1999) [1991]. A Critical and Exegetical Commentary on the Gospel According to Saint Matthew. Juz. la II: Commentary on Matthew VIII–XVIII. T&T Clark Ltd. ISBN 9780567095459. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |authormask1= ignored (|author-mask1= suggested) (help); Unknown parameter |authormask2= ignored (|author-mask2= suggested) (help)
  • Davies, William David; Allison, Dale C. (1997). A Critical and Exegetical Commentary on the Gospel According to Saint Matthew. Juz. la III: Commentary on Matthew XIX–XXVIII. T&T Clark Ltd. ISBN 9780567085184. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |authormask1= ignored (|author-mask1= suggested) (help); Unknown parameter |authormask2= ignored (|author-mask2= suggested) (help)

Vitabu vya jumla

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Injili ya Mathayo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy