Monrovia ni mji mkuu wa Liberia. Eneo uliko mji huu mwanzoni liliitwa Cape Mesurado na Wareno katika miaka ya 1560. Eneo hili lilianzwa kujenga mji mwaka 1822 na chama cha American Colonization Society ikiwa ni makazi ya watu waliokombolewa toka utumwani nchini Marekani.[1] Jina Monrovia lilitokana na jina la Rais wa Marekani James Monroe. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2003, Mji huu una wakazi wapatao 572,000.

Monrovia
Mji mkuu wa Liberia Monrovia


Jiji la Monrovia
Nchi Liberia

Uchumi wa Monrovia unategemea zaidi bandari yake na madini ya chuma. Bidhaa kama vile saruji, mafuta, matofali, vigae, samani, na kemikali zinatengenezwa Monrovia.

Historia

hariri

Wakati mabaharia Wareno walipowasilia Monrovia na kuuita mji huu "Cape Mesurado" tayari kulikuwa na wakazi wakiishi hapo. Watu wa kwanza kuhamia Monrovia toka nchini Marekani waliwasili mwaka 1822 katika Kisiwa cha Sherboro nchini Sierra Leone. Wahamiaji wengi walifariki baada ya kuwasili Monrovia.

Mkutano wa kutunga katiba ya Liberia wa American Colonization Society ulifanyikia Monrovia mwaka 1845.

  1. http://www.wdl.org/en/item/446/
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy