Yoana wa Lestonnac
Yoana wa Lestonnac, O.D.N. (Bordeaux, 27 Desemba 1556 – 2 Februari 1640) alikuwa mtawa wa Ufaransa, wa kwanza kuanzisha shirika la masista walimu (1607)[1][2].
Utotoni alikataa mahimizo ya mama yake ya kuasi Kanisa Katoliki. Baadaye aliishi miaka 24 katika ndoa, ambamo alizaa watoto watano ambao aliwalea kwa hekima baada ya kufiwa mumewe.Hatimaye, kwa mfano wa shirika la Wajesuiti, alianzisha shirika la Mabinti wa Bibi Yetu ili kulea Kikristo wasichana wengi iwezekanavyo.
Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 12 Mei 1900, halafu Papa Pius XII alimtangaza mtakatifu tarehe 15 Mei 1949.
Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka kwenye tarehe ya kifo chake[3].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Dast le Vacher de Boisville, La Vénérable Jeanne de Lestonnac et la fondation de l'Ordre des Filles de Notre Dame, (Bordeaux: R. Coussau, 1899)
- ↑ ""History of the Order of the Company of Mary, Our Lady"" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-10-07. Iliwekwa mnamo 2021-01-28.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- The Company of Mary Our Lady Official site Ilihifadhiwa 19 Machi 2017 kwenye Wayback Machine.
- Shughuli au kuhusu Yoana wa Lestonnac katika maktaba ya WorldCat catalog
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |