Content-Length: 72121 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Kamati

Kamati - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kamati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upangiliaji wa ukumbi wa kamati,1901

Kamati (kutoka neno la Kiingereza "committee") ni kundi la watu walioteuliwa au kuchaguliwa kwa ajili ya kazi maalum.

Mara nyingi huteuliwa miongoni mwa wajumbe wa kikundi au kundi kubwa na wakati mwingine hutarajiwa pia kufanya utafiti wa kina kuhusu jambo maalum kwa muda fulani na hatimaye kutoa mapendekezo kulingana na matokeo ya utafiti wao. Kwa mfano nchini Tanzania Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imeundwa chini ya Kanuni ya 118 (1) & (2) ikisomwa pamoja na fasili ya 1(c) ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016. Kwa mujibu wa fasili ya 4 (1) ya Nyongeza ya Nane, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imepewa majukumu yafuatayo: (a) Kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala yote ya haki, kinga na madaraka ya Bunge yatakayopelekwa na Spika; (b) Kushughulikia mambo yanayohusu maadili ya Wabunge yatakayopelekwa na Spika[1].

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamati kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Kamati

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy