Content-Length: 153899 | pFad | http://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi_elezo

Kamusi elezo - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Kamusi elezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Encyclopedia Britannica ilikuwa kamusi elezo mashuhuri zaidi duniani hadi kuja kwa Wikipedia.

Kamusi elezo (pia: ensaiklopidia kutoka Kiingereza: encyclopedia) ni kitabu kinachokusudiwa kukusanya ujuzi wa binadamu kadiri iwezekanavyo kulingana na wingi wa kurasa zake.

Siku hizi, Wikipedia ni kamusi elezo kubwa zaidi duniani lakini si kitabu cha karatasi, ni mkusanyo wa habari kwa umbo dijitali katika intaneti. Zamani (kabla ya kuja kwa Wikipedia) Encyclopedia Britannica ilikuwa kati ya kamusi elezo kubwa zaidi iliyokuwa ikitolewa kama vitabu vilivyochapishwa.

Historia

Katika historia yalikuwepo majaribio mbalimbali ya kukusanya ujuzi wote wa dunia. Mfano bora wa kale ni kamusi ya Yongle kutoka China iliyotungwa na wataalamu 2000 katika karne ya 14 na kuandikwa kwa mkono katika vitabu 1100.

Lakini kamusi elezo au ensaiklopedia zimekuwa na athari kubwa sana tangu Johannes Gutenberg na kupatikana kwa uchapaji wa vitabu ulioshusha kabisa bei ya vitabu kwa watu wengi.

Ensaiklopedia ya kwanza ya kisasa iliyokuwa na athira kubwa sana ilikuwa "Encyclopédie ou Dictionnaire raisonné des sciences, des arts et des métiers" iliyokusanywa na Denis Diderot pamoja na Jean Baptiste le Rond d’Alembert pamoja na waandishi zaidi ya 130 katika karne ya 18 huko Ufaransa. Kamusi elezo hii ikawa moja kati ya vyanzo vya harakati ya Zama za Mwangaza.

Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamusi elezo kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: http://sw.wikipedia.org/wiki/Kamusi_elezo

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy