Bernardo wa Corleone
Bernardo wa Corleone (Corleone, 6 Februari 1605 - Palermo, 12 Januari 1667) alikuwa bruda wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Sicilia, leo nchini Italia.
Mwaka 1768 alitangazwa na Papa Klementi XIII kuwa mwenye heri.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Yohane Paulo II tarehe 10 Juni 2001.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 12 Januari[1].
Maisha
haririFilippo Latini (alivyoitwa awali) aliingia utawa kisha kupigana na Vito Canino kwa panga mwaka 1626.
Shirikani aliishi katika konventi mbalimbali kama ifuatavyo:
- 1633: Polizzi Generosa
- 1635: Corleone
- 1636: Bivona
- 1637: Castronovo di Sicilia
- 1638: Castelvetrano
- 1639: Sambuca di Sicilia
- 1640: Bisacquino
- 1641: Ciminna
- 1642: Chiusa Sclafani
- 1643: Castronovo di Sicilia
- 1644: Agrigento
- 1646: Castronovo di Sicilia
- 1647: Caltabellotta
- 1648: Burgio
- 1650: Chiusa Sclafani
- 1651: Partinico
- 1652-1653: Palermo, alipobaki hadi kifo chake.
Katika konventi hizo alifanya toba kali na kutekeleza kwa namna ya ajabu amri ya upendo[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- [1] Ilihifadhiwa 9 Julai 2011 kwenye Wayback Machine. Tovuti rasmi ya Mt. Bernardo wa Corleone.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |