Nenda kwa yaliyomo

Barack Obama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barack Obama
Barack Obama standing in front of a wooden writing desk and two flagpoles.
6 Desemba 2012

Aliingia ofisini 
Januari 20, 2009 (2009-01-20)
Makamu wa Rais Joe Biden
mtangulizi George W. Bush
aliyemfuata Donald Trump

Muda wa Utawala
Januari 3, 2005 (2005-01-03) – Novemba 16, 2008 (2008-11-16)
mtangulizi Peter Fitzgerald
aliyemfuata Roland Burris

Mwanachama wa Seneti ya Illinois
from the 13th District
Muda wa Utawala
January 8, 1997 – November 4, 2004
mtangulizi Alice Palmer
aliyemfuata Kwame Raoul

tarehe ya kuzaliwa Agosti 4 1961 (1961-08-04) (umri 63)
Honolulu, Hawaii, U.S.
utaifa American
chama Democratic
ndoa Michelle LaVaughn Robinson (m. 1992–present) «start: (1992-10)»"Marriage: Michelle LaVaughn Robinson to Barack Obama" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Barack_Obama)
mahusiano Stanley Armour Dunham (grandfather)
Madelyn Lee Payne (grandmother)
Maya Kassandra Soetoro-Ng (half-sister)
watoto Malia Ann Obama (b. 1998)
Natasha Obama (b. 2001)
makazi Chicago, Illinois
mhitimu wa Occidental College
Chuo Kikuu cha Columbia (B.A.)
Harvard Law School (J.D.)
Fani yake Lawyer
Professor of constitutional law
Community organizer
Author
dini Ukristo
Awards Tuzo ya Nobel ya Amani
signature Barack Obama
tovuti barackobama.com

Barack Hussein Obama II (amezaliwa 4 Agosti 1961) alikuwa rais wa 44 wa Marekani. Ni Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kushika wadhifa huo, na pia mtu wa kwanza mwenye kuzaliwa Hawaii kuwa rais wa Marekani.

Obama awali alihudumu kama Seneta mdogo kutoka jimbo la Illinois, tangu Januari 2005 hadi alipojiuzulu baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008, mwezi wa Novemba.

Obama alifuzu mwanzo kutoka katika chuo kikuu cha Columbia University, kisha akafuzu katika masomo ya sheria kutoka katika kitivo cha masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Harvard, ambako alikuwa rais wa jarida la Harvard Law Review.

Alihudumu baadaye kama mwanaharakati wa mambo ya kijamii, kabla ya kuhitimu katika masomo ya kisheria.

Hatimaye, alifanya kazi kama wakili wa haki za umma mjini Chicago, kisha akafunza sheria ya kikatiba katika Chuo Kikuu cha Chicago kuanzia 1992 hadi 2004.

Obama alihudumu mihula mitatu katika Bunge la jimbo la Illinos (Illinois Senate) tangu 1997 hadi 2004. Baada ya kushindwa katika jitihada zake za kuchaguliwa katika Bunge Dogo la Marekani mwaka 2000, Obama alisimama kuchaguliwa katika Bunge La Maseneta La Marekani mwaka 2004. Alishinda uchaguzi hapo Novemba 2004.

Alitangaza kusimama kuchaguliwa kama rais wa Marekani mwezi Februari, mwaka 2007. Baada ya kampeni kali katika uteuzi wa chama cha Democratic Party dhidi ya Hillary Clinton, aliteuliwa kama mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho. Katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2008, alimshinda John McCain, aliyekuwa ameteuliwa na chama cha Republican Party, akaapishwa kama rais tarehe 20 Januari 2009.

Tarehe 9 Oktoba 2009, Obama alituzwa kwa Tuzo ya Nobel ya Amani.

Mwaka 2012 alishinda tena uchaguzi mkuu na kuendelea kuongoza hadi tarehe 20 Januari 2017, alipompisha Donald Trump.

Utoto na Ujana

Baba yake Obama alikuwa Mjaluo wa Kenya Barack Obama aliyeaga dunia 1982. Mzee Obama alitoka mkoa wa Nyanza nchini Kenya akaenda Marekani masomoni. Mama yake, Ann Dunham, alikuwa Mwamerika Mzungu kutoka jimbo la Kansas aliyeaga dunia 1995.

Wazazi walioana wakati ndoa kati ya watu weupe na weusi bado ilikuwa marufuku katika sehemu za kusini za Marekani. Wazazi waliachana baada ya miaka miwili na mtoto Barack alibaki na mama.

Baadaye mama yake aliolewa na mwanafunzi kutoka Indonesia akamfuata aliporudi kwake. Hivyo Barack aliishi Jakarta hadi 1971 aliporudi Marekani na kukaa na babu yake huko Hawaii hadi alipomaliza shule ya sekondari.

Barack ana dada mmoja kutoka ndoa ya pili ya mama yake na baba ya kambo kutoka Jakarta, Indonesia

Seneta Obama pamoja na Wangari Maathai huko Nairobi, 2006.

Masomo na kazi

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alisomea masuala ya siasa na sheria katika vyuo vya Occidental huko Los Angeles, Columbia huko New York na baadaye chuo kikuu cha Harvard. Mwaka 1991 alimaliza kwa shahada ya dokta.

Baada ya shahada ya kwanza Obama aliwahi kufanya kazi ya kijamii huko Chicago. Mwaka 1991 alirudi Chicago alipopata kazi katika ofisi ya wanasheria akafundisha pia kozi za sheria kwenye chuo kikuu cha Chicago.

Kuingia katika siasa

Mwaka 1996 alichaguliwa kama seneta wa bunge la Illinois akarudishwa 1998 na 2002. Mwaka 2004 alichaguliwa kuwa seneta wa bunge la kitaifa.

Mwezi wa Februari 2007 alitangaza ya kwamba atatafuta nafasi ya mgombea wa urais upande wa chama cha kidemokrasia. Katika kampeni ya kitaifa ndani ya chama chake alifaulu kumshinda mgombea mwenzake mama Hillary Clinton. Tarehe 28 Agosti 2008 aliteuliwa na mkutano wa chama cha kidemokrasia kuwa mgombea wa chama hicho kwa urais. Katika uchaguzi wa Novemba 2008 alimshinda mgombea wa chama cha kijamhuri seneta John McCain.

Familia

Obama alimwoa Michelle Robinson ambaye ni mwanasheria kama yeye mwenyewe. Wana mabinti wawili Malia Ann (*1998) na Natasha (*2001) anayeitwa Sasha. Familia ina nyumba yake huko Chicago.

Urais

Obama aliongoza kama rais tangu Januari 2009 hadi Januari 2017.

Tuzo ya Nobel ya Amani

Mwaka wa 2009 aliteuliwa kwa Tuzo ya Nobeli ya Amani "kwa jitihada zake za kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano kati ya mataifa".[1]

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

}}

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy