Nenda kwa yaliyomo

Baseball

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chanzo cha mchezo: mtupaji na mpiganaji wanajiandaa, mpokeaji yuko tayari
Miendo ya mtupaji (pitcher)

Baseball (mara chache pia: besibol) ni aina ya michezo ya timu yenye asili na wafuasi wengi Marekani lakini inapendwa pia na watu wengi huko Amerika Kusini na Asia ya Mashariki.

Timu mbili zinashindana kwa shabaha ya kupata ponti zaidi kuliko wengine. Asili ya baseball ni michezo iliyopelekwa Marekani na wahamiaji kutoka Ulaya. Kwa tabia kadhaa mchezo unafanana na kriketi.

Kila timu huwa na wachezaji 9. Timu zinabadilishana kwa zamu kushambulia na kutetea. Shabaha ya mchezo ni kuzunguka ("run") uwanja mwenye vituo ("base") nne. Kwa kila mafanikio ya kuzunguka uwanja timu inashika pointi moja. Timu ya wapinzani wanajaribu kuchelewesha na kuzuia wachezaji wa upande mwingine. Timu yenye pointi zaidi inashinda.

Timu ya kutetea inanza na mtupaji (pitcher) ndani ya eneo la kutupa anayetupa mpira. Analenga kwa mwenzake mshika mpira (catcher) aliye nyuma ya mpiganaji wa kinyume katika sehemu ya kupiga (strike zone) anapaswa kufikisha mpira si chini mno wala juu mno. Mpiganaji anajaribu kugonga mpira kuelekea sehemu fulani ndani ya uwanja. Kama anafaulu kugonga mpira anaanza kukimbia kuelekea kituo cha kwanza.

Kama mshika mpira aliukamata atalenga kwa mpiganaji anayekimbia ili amwondoe katika uwanja au kuiupa mpira kwa wenzaka katika uwanja watakaomlenga mchezaji anayekimbia kutoka kituo kimoja hadi kingine. Huyu akifika kituo yuko salama.

Badala yake mchezaji mwingine wa timu ya shambulio anaingia kama mpiganaji. Mchezo unarudiwa na baada ya kila pigo "hit" mpiganaji wa kwanza aajaribu kuendelea hadi kituo kinachofuata na mpiganaji wa pili anamfuata. Wakati chezaji wa kwanza wa kushambulia amefika kituo cha nne ametimiza mbio (home run) na ameshika pointi.

Kuna kanuni mbalimbali zinazoleta azimio kama mkimbiaji anaweza kuendelea au kama anatoka katika nafasi yake.

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]
Uwanja wa baseball; Sehemu za kahawia na kiibichi ni maeneo halali kwa mpira. Sehemu za buluu ni maeneo marufuku kwa mpira.
Online
  • Boswell, Thomas (Januari 18, 1987). "Why Is Baseball So Much Better Than Football?". Washington Post. Baseball Almanac. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-23. Iliwekwa mnamo 2009-05-06. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Carlin, George. "Baseball and Football". Baseball Almanac. Iliwekwa mnamo 2009-05-06.
  • Gmelch, George (Septemba 2000). "Baseball Magic". McGraw Hill–Dushkin. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-04-22. Iliwekwa mnamo 2009-09-25.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Lamster, Mark. "Baseball Before We Knew It: What's the French for 'Juiced'? (book review)", New York Times, April 10, 2005. Retrieved on 2014-06-27. 

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Ligi
Takwimu za mchezo
Hanari za baseball
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy