Nenda kwa yaliyomo

Ben Carson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Benjamin S.Carson(Kushoto)Katika ikulu ya Marekani 19/06/2008

Benjamin S. Carson (amezaliwa 18 Septemba 1951) ni daktari na mtaalamu wa Nyurolojia, pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia kwa watoto katika hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani. Alitunukiwa na rais medali ya uhuru mwaka 2008.

Historia ya elimu

[hariri | hariri chanzo]

Benjamin Solomon Carso alizaliwa katika eneo la Detroit, jimbo la Michigan. Mama yake, Sonya Carson, aliacha shule akiwa katika daraja la tatu na kuolewa na Robert Solomon Carson, aliyekuwa mchungaji mzee zaidi katika eneo la Tennesee, wakati mama yake Ben akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Wakati Carson akiwa na umri wa miaka nane tu, wazazi wake waliachana. Mama Carson aliachiwa kuwalea Benjamin na kaka yake Curtis, yeye mwenyewe. Alifanya kazi katika sehemu mbili au hata tatu kwa mara moja ili aweze kuwatosheleza watoto wake wawili. .[1]

Mwanzoni Carson alikuwa na maisha magumu shuleni,[2] hali iliyopelekea kuwa wa mwisho mara kadhaa katika darasa lake. Alikuwa akiitwa majina mbalimbali kutokana na hali hiyo, hivyo ikapelekea kukua kwa hasira kali ndani yake. Akiwa amedhamiria kubadilisha maisha ya mtoto wake, mama yake Carson akazuia muda wake wa kuangalia runinga na kumzuia kutoka nje kila siku hadi pale atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku.

Mama yake Carson alimtaka Kusoma vitabu viwili kutoka maktaba na kuandika taarifa juu ya vitabu hivyo kila wiki, bila kujali elimu yake ndogo, hata hivyo hakuweza kusoma vitu ambavyo vilikuwa vmeandikwa.

Lakini mapema, Carson alimshangaza mwalimu wake na wanafunzi wenzake kutokana na maendeleo yake. Anakumbuka “Ni wakati ule ndipo nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu” anagundua baadae. Carson anaendelea kuwashangaza wanafunzi wenzake na ndani ya mwaka mmoja alikuwa na ujuzi na kuwa katika nafasi ya juu katika darasa lake.[1]

Baada ya kugundua kuwa alitaka kuwa daktari wa magonjwa ya akili, Carson alimaliza shule na matokeo mazuri yenye heshima na hivyo alijunga na chuo kikuu cha Yale ambapo alipata shahada yake ya kwanza katika maswala ya saikolojia ya akili. Pschology. Baada ya kutoka Yale, aliendelea na shule ya udaktari ya Michigan, ambapo hapo ndipo nia yake ya kuwa daktari wa magonjwa ya akili ilipobadilika na kuwa daktari wa mishipa. Uwezo wake mkubwa wa kuona na uwezo wake wa kufikiri haraka ulimfanya awe daktari wa upasuaji mzuri zaidi. Baada ya kumaliza shule yake ya udaktari, alikuwa daktari wa mishipa msaidizi katika hospitali ya Johns Hopkins katika jimbo la Baltimore. Akiwa na umri wa miaka 33, alikuwa profesa wa hospitali na pia mkurugenzi wa idara ya upasuaji mishipa ya watoto

Kazi zake za mapema

[hariri | hariri chanzo]

Mwezi wa tisa mwaka 1987, Carson alifanya upasuaji wa kutenganisha mapacha wenye umri wa miezi saba, waliokuwa wameungana katika sehemu ya kichwa. Carson alikuwa ndiye kiongozi wa upasuaji huo mgumu.

Mwaka 1997, Carson pamoja na timu yake, walienda Afrika ya Kusini, kuwatenganisha Lukas na Joseph Banda kutoka Zambia. Watoto wote wawili waliweza kuishi baada ya upasuaji na hakuna hata mmoja wao aliyepata uharibifu wa ubongo. Watoto hao wa Banda walikuwa ni watoto wa kwanza walioungana kwa upande wa juu wa vichwa vyao kuweza kuishi baada ya upasuaji. Upasuaji huo ulifanyika kwa saa 28.

Mwaka 2003, Carson alikuwa moja kati ya madaktari waliofanya upasuaji wa watu wazima waliokuwa wameungana katika sehemu ya vichwa, Ladan na Laleh Bijan. Lakini wote hawakuweza kuishi baada ya upasuaji. Alipoulizwa kwa nini alikubali kufanya upasuaji wa kubahatisha kiasi hicho alisema, ndugu hao walikuwa wamekubali bora wafe kuliko kuendelea kuishi wakiwa wameungana.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Carson amepokea tuzo mbalimbali katika miaka mbalimbali, kama vile, Shahada za heshima za Udaktari 40, pia ni mwanachama katika chamaChuo Kikuu cha Mafanikio ya Marekani, Chama cha Wamarekani Wanajulikana wa Horatio, Alpha Omega Alpha Waheshimu Medical Society Ushirikiano wa yele, (Bodi ya wakurugenzi wa Chuo kikuu cha Yale) na mashirika mengine mengi. Pia ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Mfuko wa Somo la Carson , ambao huwasaidia wanafunzi kutoka katika historia tofauti tofauti walio na vipaji maalumu katika masomo. Mwaka 2007, Carson alijumuishwa katika Chuo kikuu cha Indiana Wesley Society ya Dunia Mabadiliko na kupokea nishani ya heshima wa udaktari wakati akizungumza katika Chuo. Aliporudi, alirudi na rafiki yake Tony Dungy ambaye naye alikumuishwa katika jamii. Tarehe 19 mwezi wa 9 mwaka 2008, Carson alopokea nishani ya raisi ya uhuru kutoka kwa Rais George W. Bush.

Utaalamu na magonjwa

[hariri | hariri chanzo]

Carson ameandika vitabu vitatu vilivoongoza katika mauzo na vilivyochapishwa na Zondervan shirika la kimataifa la uchapaji la kikristo, Vinavoitwa : Gifted Hands (Mikono Yenye Vipawa: Hadithi Ya Ben Carson), The Big Picture, na Think Big Kitabu cha kwanza cha Historia ya maisha ya mtu, na vitabu vingine viwili ni kuhusu falsafa ya maisha yake hususani katika mafanikio yake yanayoenda sambamba na imani yake kwa Mungu. Carson ni Mkristo wa kanisa la Waadventista Wasabato.

Mwaka 2002, Carson aliamuriwa kusitisha kuonekana katika maeneo yenye umati wa watu, baada ya kupata matatizo ya afya ya kwake mwenyewe. Mwezi wa sita alikutwa na dalili za kuwa na Saratani ya Kibofu cha mkojo, lakini kwa bahati nzuri, saratani hiyo iliweza kukutwa katika muda muafaka. Lakini pamoja na hayo, Carson alibadilisha mfumo wake wa maisha, Bado anafanya upasuaji kwa zaidi ya watoto mia tatu (300) kwa mwaka lakini amekuwa akijaribu kupunguza muda wake.Carson amekuwa akifanya kazi kuanzia saa 7:00 asubuhi na kumaliza saa 8:00 usiku, lakini tangu agundulike kuwa na saratani amekuwa akifanya kazi na kuondoka saa 6:15, jioni. Hii inampa muda zaidi wa kukaa na mke na watoto wake watatu.

Makala ya video kuhusu maisha ya Carson inayoitwa Gifted Hands:Kitabu kinachohusu, hadithi ya Ben Carson kilitolewa na Zondervan mwaka 1992, hali iliyopelekea mwaka 2009, filamu ya televisheni ilitolewa ikiwa na jina hilo hilo, katika TNT tarehe 07/02/2009, na kushinda tuzo ya Academi ya Gooding jr ikiongozwa na Kimberly Elise akimwelezea mama yake.[3]

Machapisho

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy