Nenda kwa yaliyomo

Felipe Solá

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gavana wa Buenos Aires
Muda aliokuwa ofisini
2002 – 2003
2003 – 2007
Naibu wake
2002-03: Hakuwa na yeyote
2003-07: Graciela Gianetassio
Kabla yake: Carlos Ruckauf
Baada yake: Daniel Scioli
Alizaliwa: 23 Julai 1950 (1950-07-23) (umri wa miaka 59)
Alipozaliwa: Buenos Aires
Chama cha Kisiasa: Justicialista
Kazi aliyosomea: Mhandisi wa Kilimo

Felipe Solá (alizaliwa 23 Julai 1950) ni mwanasiasa wa Argentina, mwanachama wa Chama cha Justicialista (wanaoendeleza siasa ya Kiperonisti) na alikuwa gavana wa jimbo la Bueons Aires hadi alipoacha ofisi hiyo katika mwaka wa 2007.

Historia ya kikazi

[hariri | hariri chanzo]

Sola ni mhandisi wa kilimo. Yeye alisoma katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires. Yeye ameoa na ana watoto wawili. Pia alikuwa:

  • profesa wa chuo kikuu,
  • mwandishi wa habari,
  • mshauri
  • mtafiti katika mada ya kiuchumi.

Wasifu wa kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Yeye alikuwa Waziri wa Masuala ya Kilimo katika serikali ya Cafiero katika jimbo la Buenos Aires(1987-1989): kisha akawa Katibu wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika utawala wa rais Carlos Menem hadi mwaka wa 1991, alikuwa naibu wa kitaifa wa jimbo la Buenos Aires. Yeye aliendelea kuhudumia katika Chemba ya Manaibu wa Taifa la Argentina hadi mwaka wa 1993,aliporejea kwenye utawala wa rais.

Rais wa Argentina Néstor Kirchner (kushoto) na gavana wa Jimbo la Buenos Aires: Felipe Solá (kulia). Picha ilipigwa 23 Oktoba 2005

Tarehe 10 Desemba 1999, yeye akawa makamu wa gavana wa Buenos Aires chini ya Carlos Ruckauf, na akachukua ugavana mnamo tarehe 3 Januari 2002 Ruckauf alipojiuzulu kutoka ugavana ili kuwa Waziri wa Masuala ya Nje.Ruckauf alienda kuwa Waziri katika serikali ya Rais Eduardo Duhalde wakati wa shida za kiuchumi na kijamii za 2001.

Felipo aliacha kuunga mkono Duhalde baada ya Néstor Kirchner kumwacha pia huku akiandaa sera zake na mipango yake kuwa sawa na za serikali ya kitaifa. Aliuunga mkono wagombea waliokuwa pamoja na Néstor Kirchner katika kampeni yake katika uchaguzi wa 2005. Katika mwaka wa 2007, baada ya kuacha ofisi ya ugavana, alikuwa tena naibu wa taifa wa jimbo lake.

Aliporudi Congress,Solá alianza kusogea mbali na uongozi wa Kirchner na kuacha muungano wao wa Front for Victory. Kabla ya uchaguzi wa Juni 2009, alikuwa akifanya kazi akiungana na Francisco de Narváez na Mauricio Macri ili kuwasilisha muungano wa Waperonisti na chama cha Republican Proposal(PRO).

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy