Jiografia ya Kenya
Jiografia ya Kenya inahusu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo ni ya 47 kwa ukubwa duniani ikifuata mara Madagaska km2 580 367 (sq mi 224 081) ikiwa na eneo la kilomita mraba 580,367 (maili mraba 224,081).
Kutoka pwani ya Bahari ya Hindi, nyanda za chini zimeinuka hadi milima ya kati. Milima hii imetenganishwa na eneo la Bonde la Ufa; sehemu tambarare yenye rutuba upande wa mashariki. Milima ya Kenya ni kati ya zilizofaulu kwa kilimo barani Afrika.
Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya (na la pili kwa urefu barani Afrika): Mlima Kenya, unaofikia urefu wa mita 5,199 (futi 17,0570) m 5 199 (ft 17 057) na ni eneo lenye mito ya barafu. Ng'ambo ya mpaka wa Tanzania Mlima Kilimanjaro (m 5 895 (ft 19 341)*) huweza kuonekana upande wa kusini.[1]
Kenya ni nchi yenye jua kali na nguo za majira ya joto huvaliwa mwaka mzima. Hata hivyo, huwa na baridi usiku na pia asubuhi na mapema.
Hali ya hewa ina joto na unyevu sehemu za pwani, joto kiasi sehemu za bara na ni kame katika sehemu za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa nchi. Hata hivyo kuna mvua nyingi kati ya Machi na Aprili, na mvua ya kadiri kati ya Oktoba na Novemba. Halijoto huwa juu zaidi miezi hii yote.
Mvua ya masika hunyesha kuanzia Aprili hadi Juni. Mvua ya vuli nayo hunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba. Wakati mwingine mvua hii huwa nyingi na aghalabu hunyesha wakati wa alasiri na jioni. Majira ya joto jingi ni kuanzia Februari hadi Machi nayo ya baridi ni Julai hadi Agosti.
Wastani wa halijoto | ||||
Mji | Mwinuko (mita) | Upeo wa juu (°C) | Upeo wa chini(°C) | |
---|---|---|---|---|
Mombasa (Mji wa Pwani) | 17 | 30.3 | 22.4 | |
Nairobi(Mji Mkuu) | 1,661 | 25.2 | 13.6 | |
Eldoret | align = "center" | 3,085 | 23.6 | 9.5 |
Lodwar (Sehemu kame nyanda za juu) | 506 | 34.8 | 23.7 | |
Mandera (Sehemu kame nyanda za juu) | 506 | 34.8 | 25.7 |
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Rough Guide Map Kenya (Ramani) (tol. la 9). 1:900,000. Rough Guide Map. Usanifu ramani wa World Mapping Project. Rough Guide. 2006. ISBN 1-84353-359-6.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jiografia ya Kenya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |