Nenda kwa yaliyomo

Nabii Eliya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nabii Eliya alivyochorwa na José de Ribera.

Eliya (kwa Kiebrania אליהו, Eliyahu, maana yake "YHWH ndiye Mungu wangu";[1] kwa Kiarabu إلياس, Ilyās), alikuwa nabii katika Ufalme wa Israeli wakati wa wafalme Ahabu na Ahazia (karne ya 9 KK).

Habari za nabii huyo maarufu sana katika Biblia, na labda katika Qurani pia, zinapatikana hasa katika vitabu vya Wafalme.

Dhidi ya uasi wa taifa la Mwenyezi Mungu, alitetea haki za Mungu pekee kwa ari kubwa hivi kwamba watu waliwafananisha naye Yohane Mbatizaji na hata Yesu mwenyewe[2].

Hakuacha maandishi, lakini kumbukumbu yake inatunzwa vizuri sana, hasa katika Mlima Karmeli.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Julai[3].

Mazingira ya kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Waisraeli walielekea dini za kandokando kwa sababu zilikuwa zinaahidi kufanikisha maombi yao kwa ibada za hakika, wakati Mungu ana hiari ya kupokea au kukataa sadaka zao. Waisraeli walijaribu kufuata pande zote mbili kwa pamoja, ila Mungu hakuweza kukubali, kwa kuwa ni peke yake tu. Imani yao iliyumba hasa wakati mfalme Ahabu alipotawala Kaskazini (869-850 hivi KK) ambapo Yezebeli, mke wake, alifanya juhudi kubwa za kuikomesha kabisa imani yao kwa YHWH ili wamuabudu Baali, mungu mkuu wa kwao aliyehusika na mvua, kufuatana na sanamu mbili zilizotengenezwa na mfalme Yeroboamu I zikiwa na sura ileile ya Baali (fahali wa dhahabu). Mezani pa malkia huyo walikuwa wanalishwa manabii wa uongo 850huyo walikuwa wanalishwa manabii wa uongo 850, kumbe manabii wa Bwana waliuawa karibu wote.

Unabii wake

[hariri | hariri chanzo]

Hapo Mungu akamtuma Eliya wa Tishbi (1Fal 17-18) ambaye jina lake lina maana ya kwamba, “Mungu wangu ni YHWH” na linajumlisha kazi yake ya kutetea kwa ari zote imani ya kweli hata akaiokoa. Ili kuondoa utata wa kuabudu pande mbili, Eliya kwanza alizuia mvua isinyeshe nchini miaka mitatu na nusu, ibada kwa Baali zisifanikiwe hata kidogo, halafu akashindana na manabii hao hadhara ya Israeli yote juu ya mlima Karmeli. Tofauti na mbinu za manabii 450 wa Baali, waliofikia kujichanja na kutoka damu ili kuvuta moto kutoka mbinguni wasifaulu, Eliya aliomba tu kwa unyofu kwamba Mungu ajitokeze ili kugeuza mioyo ya watu wake wamrudie. Kwa kuteremsha moto toka mbinguni juu ya sadaka yake YHWH alithibitisha kuwa ndiye Mungu pekee na kuwa anaendelea kuwaokoa watu wake. Baada ya Eliya kuwachinja wote aliruhusu mvua inyeshe tena. Ndiyo sababu anasifika kwa nguvu ya sala yake (Yak 5:17-18).

Hasa ni kwamba, baada ya kukimbia hasira ya Yezebeli aliyemuapia atamuua kabla ya kesho yake, akisali pangoni juu ya mlima Sinai kama Musa mwanzoni mwa agano la Israeli na Bwana, alijaliwa kutokewa na kuagizwa upya na Mungu katika sauti ndogo ya upepo mtulivu akamilishe kazi yake hasa kwa kuwafanya Elisha nabii na Yehu mfalme (1Fal 19:1-18). Hata katika Yesu kugeuka sura mlimani akatokea pamoja na Musa ili wamshuhudie kama wawakilishi wa Torati na Manabii (Mk 9:2-13).

Kwa jinsi alivyofanya kazi kwa ari, na kwa kupalizwa juu ya gari la moto (2Fal 2:1-18) akalinganishwa na moto (YbS 48:1-11) akatabiriwa atarudi kabla ya siku ya Bwana (Mal 3:23-24).

Ndiyo sababu Injili zinamtaja mara nyingi.

Sala zake

[hariri | hariri chanzo]

"Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie". (1Fal 18:36-37)

"Yatosha! Sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu". (1Fal 19:4)

Mwendelezo wa kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya wanafunzi wake (walioitwa wana wa manabii) kazi yake kwa miaka zaidi ya 50 iliyeendelezwa hasa na nabii Elisha, ambaye anasifika pia kwa miujiza yake (YbS 48:12-16) na pamoja na mwalimu wake amechukuliwa na Yesu Kristo kama mfano wa unabii wake utakaowaokoa mataifa baada ya Israeli kumkataa (Lk 4:24-27). Elisha alijihusisha sana na siasa akaombwa shauri na wafalme mbalimbali hata wa nchi za nje. Kwa kumpaka mafuta Yehu alianzisha mapinduzi dhidi ya ukoo wa Ahabu na kukomesha upotoshaji wake wa imani. Mapinduzi hayo yakaenea kusini kwa kumuua Atalia, binti wa Yezebeli, aliyetawala miaka saba kisha kuua watu wote wa ukoo wa Daudi (mtoto Yoashi tu alinusurika).

Kadiri ya Injili ya Luka, malaika Gabrieli alitabiri kuwa Yohane Mbatizaji atakayezaliwa atarithi karama ya Eliya na kutekeleza unabii wa Kitabu cha Malaki juu yake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. New Bible Dictionary. 1982 (second edition). Tyndale Press, Wheaton, IL, USA. ISBN 0-8423-4667-8, p. 319
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/63650
  3. Martyrologium Romanum

Historia

[hariri | hariri chanzo]
  • Miller, J. M. and J. H. Hayes. A History of Ancient Israel and Judah. Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 2004. ISBN 0-664-22358-3

Utamaduni

[hariri | hariri chanzo]
  • Bialik, H. N. and Y. H Ravnitzky. eds. The Book of Legends: Sefer Ha-Aggadah. New York: Schocken Books, 1992. ISBN 0-8052-4113-2
  • Ginzberg, Lewis. Legends of the Bible. Philadelphia: Jewish Publication Society of America, 1956.
  • Schwartz, Howard. Tree of Souls: The Mythology of Judaism. Oxford: Oxford University Press, 2004. ISBN 0-19-508679-1
  • Wolfson, Ron and Joel L. Grishaver. Passover: The family Guide to Spiritual Celebration. Woodstock, VT: Jewish Lights Publishing, 2003. ISBN 1-58023-174-8

Vitabu kwa watoto

[hariri | hariri chanzo]
  • Aronin, Ben and Shay Rieger. The Secret of the Sabbath Fish. Philadelphia: Jewish Publication Society of America, 1978. ISBN 0-8276-0110-7
  • Goldin, Barbara. Journeys with Elijah: Eight Tales of the Prophet. New York: Harcourt Brace, 1999. ISBN 0-15-200445-9
  • Jaffe, Nina. The Mysterious Visitor: Stories of the Prophet Elijah. New York: Scholastic Press, 1997. ISBN 0-590-48422-2
  • Jaffe, Nina. The Way Meat Loves Salt: A Cinderella Tale from the Jewish Tradition. New York: Holt Publishing, 1998. ISBN 0-8050-4384-5
  • Silverman, Erica. Gittel's Hands. Mahwah, NJ: BridgeWater Books, 1996. ISBN 0-8167-3798-3
  • Sydelle, Pearl. Elijah's Tears: Stories for the Jewish Holidays. New York: Holt Publishing, 1996. ISBN 0-8050-4627-5
  • Thaler, Mike. Elijah, Prophet Sharing: and Other Bible Stories to Tickle Your Soul. Colorado Springs, CO: Faith Kids Publishing, 2000. ISBN 0-7814-3512-9
  • Scheck, Joann. The Water That Caught On Fire. St. Louis, Missouri: Concordia Publishing House: ARCH Books, 1969. (59-1159)

Katika Qur'an

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Eliya kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy