Nenda kwa yaliyomo

Panya (Rattus)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Panya
Panya kahawia (Rattus norvegicus)
Panya kahawia (Rattus norvegicus)
Panya mweusi (Rattus rattus)
Panya mweusi (Rattus rattus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Familia ya juu: Muroidea (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na vipanya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanana zaidi na vipanya)
Jenasi: Rattus
Fischer von Waldheim, 1803
Ngazi za chini

Spishi 64, 2 katika Afrika:

Panya wa jenasi Rattus ni wanyama wagugunaji (Rodentia) wadogo kiasi wa nusufamilia Murinae katika familia Muridae ambao wana mkia mrefu. Jenasi hii ina spishi 64 lakini mbili tu hupatikana katika Afrika: panya kahawia na panya mweusi wanaotoka Asia kiasili. Spishi nyingi za Muridae huitwa panya pia na hata spishi za familia nyingine za familia ya juu Muroidea.

Spishi za jenasi Rattus zina maumbile ya kawaida ya wagugunaji. Nyingi ni nyembamba kiungalifu, ingawa nyngine ni nono. Zina pua ndefu na miguu mifupi kiasi. Zina ukubwa wa wastani na nyingi zina urefu wa mwili kati ya sm 10 na 30 na mkia wa urefu sawa au mrefu zaidi, ingawa nyingine zina mkia mfupi zaidi. Kwa kawaida huwa na uzito kati ya g 100 na 500. Takriban panya hawa wote wana rangi ya kahawia, lakini wengine wanaweza kuwa kijivu au weusi. Chini yao ni nyeupe au rangi nyingine iliyofifia. Manyoya yao ni mafupi kiasi kwa kawaida, ingawa spishi nyingine zina manyoya marefu. Mkia na nyayo za miguu zina manyoya machache au hazinayo kabisa na ni nyeupe, pinki au kahawia.

Panya wanaweza kuishi hadi miaka mitatu, lakini kwenye asilia, wengi sana huishi mwaka mmoja tu likiwa tokeo la kuwindwa na wanyama wengine, kama vile nyoka, mbweha, bundi na ndege mbuai wengine.

Panya na watu

[hariri | hariri chanzo]

Panya wengi huishi kati ya wanadamu. Hii mara nyingi husababisha uhaba wa chakula katika nchi zinazoendelea[1]. Walakini panya wasumbufu katika kundi hili ni wachache sana kwani spishi nyingi zinaishi kwenye visiwa na ziko hatarini kwa sababu ya uharibifu wa makazi yao.

Uambukizaji kwa magonjwa

[hariri | hariri chanzo]

Panya hubeba magonjwa kadhaa, ambayo wanaweza kupitisha kwa wanadamu na mamalia wengine. Kwa mfano, "Kifo Cheusi" (tauni, kilichokumba Ulaya, Afrika ya Kaskazini na sehemu za Mashariki ya Kati, kinaaminika kuwa kilisababishwa na bakteria Yersinia pestis na mwanzoni kilipitishwa na viroboto kutoka kwa panya kuelekea wanadamu. Panya pia huhusishwa na magonjwa ya mifugo kama leptospirosis, salmonellosis, toxoplasmosis n.k.

Panya wa kufugwa.

Panya wamefugwa tangu karne ya 19. Wengi sana ni panya kahawia lakini weusi pia hufugwa. Panya wafugwao wana sifa tofauti wakilinganishwa na panya mwitu kulingana na vizazi vingapi vimezalishwa[2]. Panya wafugwao pia hawaleti hatari ya ugonjwa kama mifugo mingine, kama vile paka na mbwa. Panya wafugwao huwa marafiki na wanaweza kufundishwa kutekeleza majukumu anuwai.

Panya wa Zucker.

Panya wa maabara

[hariri | hariri chanzo]

Panya hawa wafugwao walianza kutumiwa kwa majaribio ya maabara. Aina nyingi zilitengenezwa kwa uchunguzi wa magonjwa fulani. Aina moja ya panya ya maabara inajulikana kama panya wa Zucker. Panya hao huzalishwa na uwezo wa kuwa wazito kupita kiasi.

Kama chakula

[hariri | hariri chanzo]

Pengine panya wanaweza kutumiwa kwa chakula. Panya ni chanzo bora cha protini kuliko nyama nyingine. Nchini Australia Waaborijine hutumia panya katika lishe yao[3] na nchini Uhindi wanawake wa Mishmi hutumia panya kwa sababu wanaruhusiwa kula samaki na nyama ya nguruwe na panya tu[4].

Kwenye utamaduni

[hariri | hariri chanzo]
Panya weusi huruhusiwa kutembea huru kwenye Hekalu la Karni Mata

Huko Uchina panya ni mmoja wa wanyama kwenye kalenda ya Kichina ya Zodiaki. Watu waliozaliwa katika Mwaka wa Panya wanachukuliwa kuwa na sifa za panya pamoja na: ukweli, ukarimu, kiu cha kuchukua hatua, hasira ya haraka na taka. Watu waliozaliwa katika mwaka wa panya hupatana sana na watu waliozaliwa katika Miaka ya Kima na Joka na sivyo na wale wa Mwaka wa Farasi.

Kwa utamaduni wa India, mungu Ganesha hupanda panya na kwa hivyo panya huvumiliwa katika mahekalu yake. Kaskazini magharibi mwa Uhindi, katika jiji la Deshnoke, panya weusi katika Hekalu la Karni Mata wanaonyeshwa kama wanaume watakatifu. Watumishi hulisha panya kwa nafaka na maziwa. Kula chakula ambacho kimeguswa na panya inachukuliwa kama baraka kutoka kwa Mungu.

  1. Meerburg BG, Singleton GR, Leirs H (2009). "The Year of the Rat ends: time to fight hunger!". Pest Manag Sci. 65 (4): 351–2. doi:10.1002/ps.1718. PMID 19206089. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-17. Iliwekwa mnamo 2014-10-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. "Wild Rats in Captivity and Domestic Rats in the Wild". Ratbehaviour.org. Iliwekwa mnamo 2009-07-04.
  3. Hobson, Keith A.; Stephen Collier. (April 1984) Marine and Terrestrial Protein in Australian Aboriginal Diets. Current Anthropology, Vol. 25, No. 2. pp. 238-240
  4. Mills, J. P. (January 1952) The Mishmis of the Lohit Valley, Assam. The Journal of the Royal Anthropological Institute of Great Britain and Ireland, Vol. 82, No. 1. pp. 1-12
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy