Suleiman I
Suleiman I | |
---|---|
Sultani wa Milki ya Osmani | |
Suleiman I alivyochorwa na Tiziano mn. 1530 | |
Tarehe za utawala | 1520–1566 (miaka 46) |
Kusimikwa | 1520 |
Vyeo vingine | Mlinzi wa Haramain (msikiti za Makka na Madina), Khalifa, Amir al-Mu'minin |
Jina kamili | Suleiman bin Selim Khan |
Amezaliwa | 6 Novemba 1494 |
Mwenza | Roxalane |
Nasaba | Waosmani |
Suleiman I (kwa Kituruki: سلطان سليمان اول, Sultān Suleimān-i evvel au قانونى سلطان سليمان, Kānūnī Sultān Suleimān; 6 Novemba 1494 – 5 Septemba/6 Septemba 1566) alikuwa sultani wa 10 wa Milki ya Osmani. Alitawala miaka 46 kuanzia 1520 hadi 1566. Hakuna sultani mwingine aliyekaa muda mrefu kama yeye. Watu wa magharibi walimwita "Suleimani Mwadhimu"; katika dunia ya Kiislamu alijulikana kama [1] "Suleimani Kanuni" kutokana na muundo wa sheria alizorekebisha na kuunda.
Wakati wa karne ya 16 Suleimani alikuwa mtawala mashuhuri aliyeongoza milki yake hadi kufikia kwenye kilele cha uwezo na uenezaji wake. Suleimani mwenyewe aliongoza jeshi lake kuteka maboma ya Wakristo kama Belgrad, Rhodos na sehemu kubwa ya Hungaria hadi Vienna alipopaswa kurudi nyuma.
Vilevile aliteka sehemu kubwa za Mashariki ya Kati pamoja na Uajemi ya magharibi katika vita zake dhidi ya watawala Wasafawi. Afrika ya Kaskazini aliweka chini ya utawala wake hadi Algeria. Jeshi la maji la Waosmani lilitawala Mediteranea, Bahari ya Shamu na Ghuba ya Uajemi. Katika bahari Hindi Waosmani walipagana na Wareno na kutuma wanmajeshi hadi Aceh katika Indonesia.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Merriman.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "1548-49". The Encyclopedia of World History. 2001. Iliwekwa mnamo 2007-04-18.
- "1553-55". The Encyclopedia of World History. 2001. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-30. Iliwekwa mnamo 2007-04-18.
- "A 400 Year Old Love Poem". Women in World History Curriculum Showcase. Iliwekwa mnamo 2007-04-18.
- Embree, Mark (2004). "Suleiman The Magnificent". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-30. Iliwekwa mnamo 2007-04-18.
- Halman, Talat (1988). "Suleyman the Magnificent Poet". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-03-09. Iliwekwa mnamo 2007-04-18.
- "The History of Malta". 2007. Iliwekwa mnamo 2007-04-27.
- Hope, Maggie. "Suleiman The Magnificent". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-04-04. Iliwekwa mnamo 2007-04-18.
- "Muhibbî (Kanunî Sultan Süleyman)". Türkçe Bilgi—Kim kimdir? (kwa Turkish). Iliwekwa mnamo 2008-01-13.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - Russell, John (2007-01-26). "The Age of Sultan Suleyman". New York Times. Iliwekwa mnamo 2007-08-09.
{{cite news}}
: Check date values in:|date=
(help)
Soma pia
[hariri | hariri chanzo]- Bridge, Anthony (1983). Suleiman the Magnificent, Scourge of Heaven. New York: F. Watts. OCLC 9853956.
- Downey, Fairfax Davis. The Grand Turke, Suleyman the Magnificent, sultan of the Ottomans. New York: Minton, Balch & Company. OCLC 25776191.
- Hooker, Richard. "The Ottomans: Suleyman". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1999-01-17. Iliwekwa mnamo 2007-09-02.
- Lybyer, Albert Howe (1913). The government of the Ottoman empire in the time of Suleiman the Magnificent. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press. OCLC 1562148.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Sultan Suleyman Tomb Ilihifadhiwa 24 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.