Nenda kwa yaliyomo

Ufalme wa Buyeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Buyeo (부여, Karne ya 2 KK - 494) au Puyŏ (Tamka pujʌ), Fuyu kwa Kichina, ulikuwa ufalme wa kale wa Korea uliopo kwenye Manchuria ya leo kaskazini mwa nchi ya Korea Kaskazini, kunako karne ya 2 KK hadi 494. Mabadiki yake yaka-fyonzwa na ufalme wa jirani na ndugu zao Goguryeo mnamo 494. Wote Goguryeo na Baekje, ni Falme Tatu za Korea, wote wawili wanajihesabu kama warithi wa taifa.

Japokuwa rekodi zenyewe kwa zenyewe zinapingana, imedhaniwa kwamba mnamo 86 KK, Dongbuyeo (Buyeo Mashariki) imeanzisha tawi lake, baada ya ile Buyeo ya awali kuna kiopindi kuitwa kama Bukbuyeo (Buyeo Kaskazini). Jolbon Buyeo iliendelea kuwa Bukbuyeo chini ya jina jipya la nchi. Mnamo 538, muda mrefu baada ya kuanguka kwa Buyeo, Baekje ikabaki kama ilivyo Nambuyeo (Buyeo Kusini).

"Buyeo" inaweza kutaja jina la ukoo la Baekje au Jimbo la Buyeo huko mjini Korea Kusini.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Chimbuko

[hariri | hariri chanzo]
Proto-Three Kingdoms, c. 001 AD.

Mwanzilishi wa ufalme wa Buyeo huenda akawa Dongmyeong, hakuwa na uhusiano na Jumong aliyeanzisha Goguryeo. Baada ya kujenga msingi wake, Hae Mosu (해모수, 解慕漱:mtoto wa miungu) na kuleta mahakama ya kifalme kwenye mjengo wake mpya, na kumtangaza kama mfalme. Hae Mosu akaita ufalme mpya jina la "Buyeo" kuonyesha kwamba yeye ndiye alikuwa mrithi wa kweli wa Wafalme wa Buyeo.

Jumong anaelezewa kuwa kama mtoto wa Hae Mosu na Yuhwa (유화, 柳花), ambaye alikuwa binti wa Habaek (하백, 河伯).

Dongbuyeo

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Dongbuyeo

Kwa mujibu wa Samguk Sagi na akaunti nyingine, ufalme wa Dongbuyeo (86 KK - 22 CE) wakaanzisha matawi yao huko mjini mashariki mwa Bukbuyeo, karibu na nchi ya Okjeo. Mfalme wa Bukbuyeo alikufa, na ndugu yake Hae Buru akarithi cheo na akawa mfalme wa Bukbuyeo.

Hae Buru akampata chura wa dhahabu chini ya jabari kubwa. Hae Buru akamwita mtoto wake Geumwa, maana yake chura wa dhahabu, na kisha baadaye akamfanya kuwa mtoto mkubwa wa mfalme.

Geumwa akawa mfalme baada ya kifo cha Hae Buru. Geumwa akakutana na Yuhwa, binti wa Habaek, na kumleta mjengoni kwake. Akasema kwamba amepata ujauzito kwa mwanga wa jua na kutaga yai la dhahabu. Geumwa amefanya majaribio kadhaa ya kuliangamiza yai lile, lakini hakufaulu, na kulirudisha lile yai kwa Yuhwa. Kutoka kwenye yai likatotoa Jumong, ambaye baadaye akajakuanzisha ufalme wa Goguryeo. Jumong baadaye akakimbilia Jolbon Buyeo baada ya majaribio kadhaa ya kutaka kumwua kutokea yaliyofanywa na watoto saba wa Mfalme Geumwa.

Mtoto mkubwa wa Geumwa (Daeso) akawa mfalme aliyemfuata. Daeso akaivamia Goguryeo wakati wa utawala wa pili wa Mfalme Yuri. Mfalme wa tatu wa Goguryeo (Mfalme Daemusin) akaishambulia Dongbuyeo na hatimaye kumwua Daeso. Baada ya fitina za ndani kwa ndani, Dongbuyeo ikaanguka, na eneo lake likachukuliwa na Goguryeo.

Mabishano, Nguzo ya Habari ya Gwanggaeto imetaja kwamba Dongbuyeo ilikuwa nchi ya shari ya Goguryeo, hata baada ya muda mrefu wa kuangamizwa kwake. Kwa kuwa mwenendo wa Samguk Sagi kutokuwa thabiti, Dongbuyeo wakataja kwenye ubao wao wa habari na umedhaniwa na wanahistoria wengi kwamba kulikuwa na migongano ya kiharakati na Dongbuyeo, iliundwa 285.

Jolbon Buyeo

[hariri | hariri chanzo]

Rekodi nyingi za kihistoria zinataja jina la “Jolbon Buyeo” (졸본부여, 卒本夫餘), dhahili linamaanisha Goguryeo au mji wake mkuu.

Mnamo 37 KK, Jumong akawa mfalme wa kwanza wa Goguryeo. Jumong akaenda kuichukua na Okjeo, Dongye, na Haengin, kwa kuzirerejesha baadhi ya maeneo ya zamani ya Gojoseon.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy