Wimbisauti
Mandhari
Wimbisauti (au: wimbi la sauti) ni njia ya uenezaji wa sauti katika nafasi.
Kwa macho ya fizikia "sauti" ni mtetemo wa gimba (kwa mfano utando) unaoendelea kama wimbi katika midia ulipo. Kwa macho ya fiziolojia na saikolojia "sauti" ni mapokezi ya wimbisauti kwa milango ya fahamu hasa sikio na utambuzi wake katika ubongo.
Wimbisauti na midia
[hariri | hariri chanzo]Wimbisauti ni wimbi mekanika yaani inahitaji midia inapoenea. Haiwezi kuenea katika ombwe. Kimsingi ni wimbi la shinikizo lililosababishwa na mtetemo wa gimba asilia halafu mtetemo huu unaendelea katika midia kama ufuatano wa vipindi vifupi vya shinikizo juu na duni katika
- gesi, kwa mfano hewa: mtetemo katika kikoromeo shingoni unatikisisha hewa na kutoka nje kupitia hewa ya nafasi tuliko
- kiowevu, kwa mfano maji: kama chuma inagongwa kwa nyundo chini ya maji mtetemo wake unaendelea katika maji; mtu mwenye kichwa chini ya maji anasikia sauti hii. Nyangumi wanawasiliana kwa kuimba chini ya maji, mtetemo wa sauti ao unasafiri kwa njia ya mawimbi ya shinikizo ndani ya maji.
- dutu mango, kwa mfano gimba la metali: kama bomba ndefu inagongwa sauti yake inasikika kwa kuweka sikio moja kwa moja juu ya bomba hata kwa umbali mkubwa.
Kasi ya wimbisauti ni tofauti kutegemeana na midia inapopita.
- ndani ya hewa yenye sentigredi 20 sauti inatembea mita 343 kwa sekunde, yaani kilomita 1 kwa sekunde 3, au takriban kilomita 20 kila dakika.
- ndani ya maji ya bahari sauti inatembea mita 1,500 kwa sekunde, hivyo takriban kilomita 90 kila dakika.
- ndani ya gimba la chuma sauti inatembea mita 5160 kwa sekunde, hivyo takriban kilomita 300 kila dakika (kama bomba au pau ndefu vile ya chuma ipo)
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Wikibooks has a book on the topic of |
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikisource has original text related to this article: |
- What is a soundwave? Archived 20 Machi 2015 at the Wayback Machine.
- Sound is a pressure wave (physisclassroom)
- Sound Wave Characteristics (Physics for kids)
- Sounds Amazing; a KS3/4 learning resource for sound and waves Archived 13 Machi 2012 at the Wayback Machine.
- HyperPhysics: Sound and Hearing
- Introduction to the Physics of Sound
- Hearing curves and on-line hearing test
- Audio for the 21st Century Archived 23 Januari 2009 at the Wayback Machine.
- Conversion of sound units and levels
- Sound calculations
- Audio Check: a free collection of audio tests and test tones playable on-line
- More Sounds Amazing; a sixth-form learning resource about sound waves Archived 17 Juni 2014 at the Wayback Machine.