Nenda kwa yaliyomo

Yosia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Yosia akisomewa sheria za Mungu zilizopatikana hekaluni.

Yosia (kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana yake "aliyeponywa na YHWH" au "aliyetegemezwa na Yah"[1][2]; kwa Kigiriki: Ιωσιας; kwa Kilatini: Josias; 649 KK609 KK) alikuwa mfalme wa 16 wa Yuda (641 KK – 609 KK) aliyejitahidi kufanya urekebisho upande wa dini ya Israeli ili kufuata zaidi Torati iliyoelekea kukamilika wakati huo, kwa mchango wake pia.

Hasa alitumia nguvu zake zote kutekeleza agizo la gombo lililopatikana mwaka 622 KK likidai sadaka zote zitolewe katika hekalu la Yerusalemu tu, kadiri ya msimamo wa Kumbukumbu la Torati: "Mungu mmoja, hekalu moja".

Ndiyo maana Biblia inamsifu kwa namna ya pekee pamoja na Hezekia kati ya wafalme wote wa Israeli na Yuda, mbali na Daudi aliyebaki kielelezo cha kudumu cha mtawala aliyempendeza Mungu.

Mwana wa mfalme Amon na Jedidah[3], Yosia alirithi utawala akiwa mtoto wa miaka 8 tu, kutokana na uuaji wa baba yake, akatawala miaka 31,[4] kuanzia 641/640 KK hadi 610 KK/609 KK.[5]

Anatajwa pia katika Injili ya Mathayo (1:10-11) kati ya mababu wa Yesu.

Lakini nje ya Biblia hatajwi popote.[6]

Babu yake, Manase anatajwa na Biblia kama mmojawapo kati ya wafalme waovu zaidi wa ukoo wa Daudi kwa jinsi alivyoelekeza raia zake kuacha ibada ya Mungu mmoja ili kufuata dini za mataifa makuu ya wakati huo, hata kutumia Hekalu la Yerusalemu, kinyume cha uaminifu wa baba yake Hezekia.

Yosia alizaa watoto wa kiume wanne: Yohane, Eliakimu[7], Matania na Shalumu.[8]

Kwanza Shalumu alimrithi Yosia kwa jina la Yehoahazi.[9] lakini baada ya miezi miatu tu nafasi yake ilishikwa na Eliakimu kwa jina la Yehoyakimu,[10] halafu na mtoto wa huyo, Yekonia;[11] hatimaye alitawala Matania kwa jina la Sedekia.[12] Huyo akawa mfalme wa mwisho wa Yuda kwa kushindwa na Babuloni aliyoisaliti, akapelekwa uhamishoni huko pamoja na Wayahudi wengi mwaka 586 KK.

Urekebisho

[hariri | hariri chanzo]
Ua wa ndani wa Hekalu la Solomoni.

Kwa miaka 13 tu (622 - 609 K.K.) Yosia alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya Waisraeli wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mwenyezi Mungu sadaka nje ya hekalu la Yerusalemu.

Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha nabii Nahumu (612 hivi K.K.).

Lakini Yosia alipokufa vitani kabla ya wakati mambo yakaharibika haraka sana, kwa sababu urekebisho ulitokana zaidi na juhudi zake binafsi, mbali ya kuungwa mkono na watu wachache kama nabii Yeremia.

  1. Josiah definition - Bible Dictionary - Dictionary.com. Retrieved 25 July 2011.
  2. Wells, John C. (1990). Longman pronunciation dictionary. Harlow, England: Longman. uk. 386. ISBN 0-582-05383-8. entry "Josiah"
  3. "Josiah", Jewish Encyclopedia
  4. 2Fal 22:1; 2Fal 21:23-26; 2Fal 21:26
  5. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257, 217.
  6. Alpert, Bernard; Alpert, Fran (2012). Archaeology and the Biblical Record. Hamilton Books. uk. 74. ISBN 978-0761858355.
  7. 2 Kings 23:34
  8. 1Nya 3:15; 2Fal 23:36; 2Fal 24:18; 2Fal 23:31
  9. 1Nya 3:15; Yer 22:11
  10. 2Nya 36:4;
  11. 2Nya 36:8
  12. 2Fal 24:17

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy