Content-Length: 140994 | pFad | https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Msimamo_wa_kutopendelea_upande

Wikipedia:Msimamo wa kutopendelea upande - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Msimamo wa kutopendelea upande

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msimamo wa kutopendelea upande wowote ni sheria ya msingi kwa watu wote wanaochangia humo kuandika au kusahihisha makala.

Maana yake ni kwamba wakati wa kutunga makala waandishi hawatakiwi kuonyesha ya kwamba wanapenda au kutopenda habari ndani ya makala. Inasaidia kuangalia kama kuna hoja juu ya kichwa zinazokubaliwa na watu wengi na pia na wataalamu.

Tuanze kwenye hoja zinazokubaliwa na wengi

Ni muhimu kuonyesha yale ambako wengi sana wanaweza kukubaliana na kutaja baadaye tu yale ambako watu hutofautiana. Pale ambako mawazo ya kitaalamu yanatofautiana makala haitakiwi kuchukua upande wowote lakini kuonyesha sifa na kasoro za kila upande. Lakini kwa kawaida tofauti hizi zisiwe mkazo wa makala.

Wakati mwingine ni rahisi kutopendelea upande fulani lakini wakati mwingine ni vigumu. Mara nyingi inasaidia kupeleleza mawazo ya kitaalamu na kuonyesha vyanzo kwa ajili mawazo yale ya kitaalamu.

Mapatano ya wengi hayana uhakika ya ukweli

Kukubaliana na watu wengi hakuondoi matatizo yote. Inatokea ya kwamba watu wengi sana hukubaliana kuamini habari isiyo kweli. Mapatano si lazima kuwa ukweli. Hapa ni sharti kupeleleza habari halisi na kutafuta vyanzo.

Hapa penye Wikipedia ya Kiswahili tutaangalia mara nyingi yale yaliyoandikwa katika Wikipedia ya Kiingereza. Lakini hii haina maana kwamba yale yaliyo kule ni "ukweli" au habari halisi.

Sahihisho mfululizo

Kuhusu hizi mada ngumu Wikipedia ina faida ya kuwa kamusi iliyo wazi inayoweza kusahihishwa tena na tena.

Makala kuhusu habari za siasa, dini, itikadi

Makala kuhusu mada haiwezi kudai ukweli wa imani au maoni fulani. Ni vizuri kueleza msimamo wa wafuasi wa dini au siasa fulani, lakini ni lazima kuonyehsa pia mitazamo tofauti au ukosoaji.

Mfano wa hoja zisizopatana na kutafuta msimamo wa kutopendelea

Watu wakijadiliana habari za viongozi, wanasiasa, dini n.k. wanaweza kutofautiana juu ya mengi.

Mfano wa mfalme XYZ

Mfano: Mfalme XYZ. Wengine watasema alikuwa mtu mbaya aliyeanzisha vita na kuua watu wengi. Wengine wanaweza kumwona kama mfalme bora aliyejitahidi kutunza amani lakini alilazimishwa na maadui kujitetea. Kwa hiyo upande mmoja wanamkumbuka kuwa mfalme mwema lakini wengine wanamwita mfalme mbaya.

Kukusanya habari halisi zinazokubaliwa na karibu wote

Hata hivyo pande zote mbili ZInaweza kupatana juu ya habari halisi kama vile:

  1. alizaliwa mwaka 1910
  2. wazazi wake waliitwa ABC na KLM
  3. alitawala nchi ya DEF.
  4. aliongoza nchi yake katika vita muhimu vya 1932 - 1935
  5. alikufa kutokana na ajali ya gari lake.

Kama karibu watu wote hukubaliana juu ya habari hizi basi tumeshapata msingi wa kutunga makala kufuatana na msimamo wa kutopendelea.

Kutaja habari zisizokubaliwa na wote

Baadaye tunaweza kuongeza habari zake zisizokubaliwa na wote, kwa mfano:

  1. alisifiwa mara nyingi kwa sababu aliamuru kujengwa kwa majengo mazuri katika mji mkuu anakumbukwa kama mjenzi mkuu wa taifa. Lakini wengine wanadai eti mipango yote yalianzishwa tayari wakati wa babake aliyemtangulia na mbunifu wa baba aliwajibika kwa uzuri wa kazi.
  2. wataalamu wa magharibi ya nchi husema alijenga umoja wa taifa na kusambaza lugha ya kitaifa. Lakini wataalamu wa mashariki wa nchi husema ya kwamba aikandamiza vikali utamaduni wa sehemu ile pamoja na wasemaji wa lugha ya mashariki na kuwaua wengi walijaribu kuwafundisha watoto wao.
  3. watalaamu watetezi wake wanasema alifaulu kutetea taifa dhidi ya tishio la nchi jirani kwa njia ya vita; lakini wengine wamegundua nyaraka zake inapoonekana ya kwamba alipanga kwa siri kushambulia nchi jirani akalipa wanasiasa wa huko kutamka tishio dhidi ya nchi yake

Kama una wasiwasi juu ya makala kama ina mwelekeo wa upande mmoja unaweza kutaja sababu zako kwenye ukurasa wa majadiliano na kubandika maandishi ya {{upendeleo}} juu ya makala. Baadaye sanduku itaonekana juu ya ukurasa wa makala husika inayosema ya kwamba Mwanawikipedia anadhani ya kwamba
makala hii hailingani na msimamo wa kutopendelea upande. Swali hili laweza kujadiliwa kwenye ukurasa wa majadiliano.

Hapa watumiaji wengine wataangalia makala hii hasa na kuchangia kwenye swali linalijadiliwa.

Kutofautisha mawazo na habari halisi

Bwana Juma ni mwanamichezo maarufu anapendwa na wengi pia na wanawikipedia.

  1. Si sawa kuandika "Juma ni mwanamichezo bora nchini Kenya". Hii ni mawazo tu na msomaji haiwezi kujua eti kipimo cha ubora ni nini.
  2. Kinyume chake inawezekana kuandika "Juma amepata medali nyingi katika historia ya michezo ya Kenya" maana hii ni habari halisi inayoweza kuthebitishwa au kupingwa.
  3. Wakati mwingine inawezakana kuandika "Juma anatazamiwa na Wakenya wengi kama mwanamichezo bora wa nchi" kama uthebitisho fulani unapatikana; kwa mfano kura ya maoni ya gazeti fulani inayotajwa kama chanzo kwenye maelezo chini ya makala; au "Juma ametajwa na rais wa nchi kama mwanamichezo bora..." ambayo inahitaji pia dondoo kama chanzo.

Vigezo

Hiki ni kigezo husika {{Upendeleo}} :


Pamoja na maelezo ya ziada inaweza kuonekana hivi

{{Upendeleo|date=Septemba 2010}}

Kigezo hiki kinaweza kutumiwa pia kwa kifupi cha Kiingereza {{POV}} :

("point of view")








ApplySandwichStrip

pFad - (p)hone/(F)rame/(a)nonymizer/(d)eclutterfier!      Saves Data!


--- a PPN by Garber Painting Akron. With Image Size Reduction included!

Fetched URL: https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Msimamo_wa_kutopendelea_upande

Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy