Kitabu cha Yuditi

(Elekezwa kutoka Kitabu cha Yudith)

Kitabu cha Yudith ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Michelangelo Buonarroti, Yuditi na kichwa cha Oloferne, 1508-1512, Cappella Sistina, Vatikano.

Kimo katika Septuaginta na katika Agano la Kale la Kanisa Katoliki, la Waorthodoksi wengi na la baadhi ya Waprotestanti, lakini si katika Tanakh ya Uyahudi wala katika Biblia ya Waprotestanti.

Habari iliyomo

hariri

Hadithi hiyo, iliyoandikwa katika karne ya 1 KK inahusu wakati wa mfalme Nebukadreza II, na vita vyake dhidi ya Israeli (karne ya 6 KK).

Kinyume cha matarajio, Yudith, ambaye jina lake linamaanisha mwanamke wa kabila la Yuda, aliweza kupata ushindi mkubwa dhidi ya maadui wa taifa la Israeli kwa imani na ushujaa wake.

Habari hiyo ya ajabu ilipata mwangwi kwa wingi katika sanaa mbalimbali.

Ufafanuzi

hariri

Wengi wanaona katika Yuditi kielelezo cha Bikira Maria katika mapambano dhidi ya shetani, hasa kutokana na maneno yafuatayo: "Umebarikiwa, binti yangu, usoni pa Mungu Aliye Juu, kuliko wanawake wote duniani. Na ahimidiwe Bwana Mungu, Muumba mbingu na nchi, aliyekuongoza hata ukampiga kichwa mkuu wa adui zetu" (Yudith 13:18).

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Yuditi kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy