Nenda kwa yaliyomo

Abdulrazak Gurnah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abdulrazak Gurnah

Abdulrazak Gurnah Al Kindi (amezaliwa Zanzibar, 20 Desemba 1948[1] ) ni mwandishi mwenye asili ya Zanzibar aliyeishi nchini Uingereza tangu mwaka 1968. Huko anafundisha katika Chuo Kikuu cha Kent tangu mwaka 1982.

Tangu mwaka wa 1987 alitolea riwaya kadhaa kwa lugha ya Kiingereza. Mwaka 2021 alipewa tuzo ya Nobel ya Fasihi[2][3].

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Abdulrazak Gurnah alizaliwa katika Usultani wa Zanzibar, ambao kwa sasa ni sehemu ya Tanzania.[4] Alifika Uingereza mwaka 1968 baada ya kukimbia Zanzibar kutokana na machafuko yaliyowalenga watu wenye asili ya Kiarabu wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar. [5][6] Gurnah amewahi kusema, 'Nilikuja Uingereza wakati ambao maneno kama "asylum-seeker" hayakuwa yakitumika sana kama wakati huu, watu wengi zaidi wanateseka na kukimbia nchi za kigaidi.'[7] [8]

Alipofika Uingereza alianza kusoma kwenye Chuo cha Christ Church College, Canterbury, baadaye akahamia Chuo Kikuu cha Kent alipopata shahada ya uzamili katika fasihi mnamo 1982. Tasnia yake ilikuwa kuhusu Criteria in the Criticism of West African Fiction.

Kuanzia mwaka 1980 hadi 1983, Gurnah alifundisha kwenye Chuo Kikuu cha Bayero mjini Kano, Nigeria. Akarudi Uingereza akawa profesa wa fasihi hadi alipostaafu [9].

Kazi zake

[hariri | hariri chanzo]

Hadithi nyingi zilizosimuliwa na Gurnah zinaonyesha mazingira ya pwani ya Afrika ya Mashariki, na wahusika wakuu wa riwaya zake ni wenyeji wa Unguja. Mhakiki wa fasihi Bruce King aliona kwamba Gurnah anaonyesha wahusika wake Waafrika katika uhusiano mpana na Dunia yote, akiwaona kama sehemu za Dunia kubwa inayoendelea kubadilikabadilika. Kufuatana na King, wahusika wa Gurnah mara nyingi ni watu walioondolewa katika asili zao, wanaokataliwa na jamii na kujisikia kama wahanga wa maisha[10]. Mhakiki Felicity Hand aliona kuwa riwaya za Admiring Silence, By the Sea na Desertion, zote zinajadili hisia za kuwa mgeni na kukosa ndugu zinazotokea kwa watu waliopaswa kuondoka kwao na kukaa ugenini. [11]

Tuzo na heshima

[hariri | hariri chanzo]

Gurnah ndiye mshindi wa tuzo ya Nobel ya fasihi ya mwaka 2021. [12][13] Alichaguliwa kuwa mmoja wa wanajumuiya ya kitaaluma ya fasihi ya Royal Society of Literature mwaka 2006.[14] Mwaka 2007 alishinda tuzo ya RFI Witness of the world nchini Ufaransa kupitia riwaya yake ya By the Sea.[15]

Tuzo nyingine alizowahi kushinda ni pamoja na tuzo ya waandishi wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Writers Prize (Eurasia Region, Best Book)) mwaka 2006, tuzo ya kitabu ya Los Angeles Times kwenye kundi la tamthiliya mwaka 2001 na tuzo ya Booker mwaka 1994.[16]

Orodha ya riwaya zake

[hariri | hariri chanzo]
  1. Loimeier, Manfred (2016-08-30). "Gurnah, Abdulrazak". Katika Ruckaberle, Axel (mhr.). Metzler Lexikon Weltliteratur: Band 2: G–M (kwa Kijerumani). Springer. ku. 82–83. ISBN 978-3-476-00129-0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2021.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. https://www.nobelprize.org/prizes/literature/2021/summary/
  3. https://www.nobelprize.org/prizes/literature/2021/press-release/
  4. King, Bruce (2004). Bate, Jonathan; Burrow, Colin (whr.). The Oxford English Literary History. Juz. la 13. Oxford: Oxford University Press. uk. 336. ISBN 978-0-19-957538-1. OCLC 49564874.
  5. Flood, Alison. "Abdulrazak Gurnah wins the 2021 Nobel prize in literature", The Guardian, 2021-10-07. (en) 
  6. "Nobel Literature Prize 2021: Abdulrazak Gurnah named winner", BBC News, 2021-10-07. (en-GB) 
  7. BBC (October 7, 2021) Nobel Literature Prize 2021: Abdulrazak Gurnah named winner Retrieved 7 October, 2021
  8. Prono, Luca (2005). "Abdulrazak Gurnah - Literature". British Council. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Agosti 2019. Iliwekwa mnamo 2021-10-07.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Flood, Alison (7 October 2021). "Abdulrazak Gurnah wins the 2021 Nobel prize in literature". The Guardian. Archived from the original on 7 October 2021. Retrieved 7 October 2021.
  10. King, Bruce (2006). "Abdulrazak Gurnah and Hanif Kureishi: Failed Revolutions". In Acheson, James; Ross, Sarah C.E. (eds.). The Contemporary British Novel Since 1980. New York: Palgrave Macmillan. pp. 85–94. doi:10.1007/978-1-349-73717-8_8. ISBN 978-1-349-73717-8. OCLC 1104713636.
  11. https://www.tandfonline.com/doi/abs/10.1080/00111619.2014.884991 Felicity Hand, Searching for New Scripts: Gender Roles in Memory of Departure
  12. "Abdulrazak Gurnah wins the 2021 Nobel prize in literature". 7 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2021. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |1= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Tanzanian novelist Gurnah wins 2021 Nobel for depicting impact of colonialism, migration". 7 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Abdulrazak Gurnah" (kwa Kiingereza (Uingereza)). Royal Society of Literature. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 7 Oktoba 2021. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Abdulrazak Gurnah, Prix RFI Témoin du Monde 2007". RFI (kwa Kifaransa). 8 Machi 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 8 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  16. "Abdulrazak Gurnah". Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2021. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |1= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abdulrazak Gurnah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy