Juan Manuel Santos
Juan Manuel Santos Calderón (alizaliwa 10 Agosti 1951) ni mwanasiasa nchini Kolombia. Mwaka 2010 alikuwa rais [1] akifuatana na mtangulizi wake Álvaro Uribe. Katika serikali ya Uribe alishika ofisi ya waziri wa ulinzi.
Tangu kuwa mkuu wa serikali Calderon alijaribu kusaidia maskini na hasa kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe katika sehemu kubwa za nchi yake. Alianza majadiliano na kundi la wanamgambo ya FARC na kufikia mapatano ambako wanachama FARC watasamehewa makosa na mashtaki yote, wanahidiwa viti 10 bungeni na kukabidhi silaha kwa serikali.
Mapatano haya yalipowekwa mbele ya wananchi katika kura yalikataliwa kwa kura 50,000 kitaifa[2] kwa sababu upinzani dhidi ya msamaha kwa jinai zilizotekelezwa na FARC.
Hata hivyo kazi ya Santos iliwahi kuangaliwa na kamati ya Nobel. Kamati ya Tuzo ya Nobel ya Amani iliamua kumkabidhi rais Santos tuzo ya amani hata baada ya kujua matokeo ya kura.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Historical Challenge". Semana International. 13 Agosti 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-01-19. Iliwekwa mnamo 19 Agosti 2010.
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Colombia referendum: Voters reject Farc peace deal BBC News, 3 October 2016
- ↑ "The Nobel Peace Prize 2016 - Press Release". www.nobelprize.org. Iliwekwa mnamo 2016-10-07.
Makala hii kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobel bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Juan Manuel Santos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |