Nenda kwa yaliyomo

Nguruwe-kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nguruwe-kaya
Nguruwe-kaya
Nguruwe-kaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili))
Nusuoda: Suina
Familia: Suidae (Wanyama walio na mnasaba na nguruwe)
Nusufamilia: Suinae (Nguruwe)
Jenasi: Sus
Spishi: S. scrofa
Nususpishi: S. s. domestica
Linnaeus, 1758

Kutoka Wikipedia, ensaiklopidia huru

Nguruwe-kaya ni kundi la wanyama wanaofugwa kote duniani. Kibiolojia ni nususpishi ya Sus scrofa. Jumla ya nguruwe duniani hukadiriwa kuwa bilioni mbili.

Nguruwe hufikia uzito wa kilogramu 40–350. Kichwa kinaishia katika mdomo mrefu unaofanana kidogo na mwiro wa tembo ingawa ni mfupi.

Wataalamu wanaona asili ya nguruwe kwenye mabara ya Afrika, Asia na Ulaya. Spishi nyingi ziko Asia.

Nguruwe ni mlawangi mmaana yake anakula kila kitu: majani, manyasi, matunda, wadudu, ndege au wanyama wengine.

Kwa kawaida nguruwe anafugwa kwa nyama yake lakini pia ngozi ina matumizi yake. Nyama ya nguruwe ni nyama inayoliwa sana Ulaya na pia Asia ya mashariki na kusini-mashariki. Katika tamaduni kadhaa nguruwe na nyama yake hutazamiwa kuwa najisi, kwa mfano katika Uyahudi na Uislamu.

Nguruwe ni mnyama mwenye akili sana akilingana na mbwa. Nguruwe

ni mnyama mwenye pua kubwa, macho madogo na mkia mdogo unaokuwa umejikunja na mfupi, uliopinda au ulionyooka. Huwa ana mwili mkubwa, miguu mifupi na nywele zilizojiviringisha. Ana kwato nne kwa kila mguu, huku mbili kubwa za mbele zikitumika kutembelea.

Kuzaa huwezekana msimu wote wa mwaka katika ukanda wa tropiki, lakini hasa misimu ya mvua. Nguruwe jike huweza kubeba mimba akiwa na miezi 8 mpaka 18. Kisha ataanza kupata hedhi kwa muda wa siku 21 kama hajashika mimba.

Nguruwe dume huweza kushiriki masuala ya uzazi katika umri wa miezi 8 mpaka 10. Kwa uzao mmoja, wanaweza kupatikana watoto 6 mpaka 12, waitwao vibwagala. Kisha kuachishwa kunyonya, familia mbili au tatu zinaweza kuishi pamoja mpaka msimu mwingine wa kujamiiana.

Nguruwe hawana tezi za jasho, hivyo nguruwe hujipoza kwa kutumia maji au matope wakati wa joto kali. Pia hutumia matope kama njia ya kujikinga na kuunguzwa na jua. Zaidi, matope huzuia wasiathiriwe na inzi na vijidudu.

Nguruwe wanaofugwa nyumbani hukuzwa na wakulima kwa ajili ya nyama na ngozi. Nywele zao ngumu hutumika pia kwa kutengeneza brashi. Baadhi ya aina za nguruwe, kama vile wale wa Asia, "pot-bellied pig", huwekwa kama wanyama wa ndani wapenzi.

Nguruwe ni 'Omnivora', yaani wanakula nyama na majani. Nguruwe hula mabaki na hujulikana kwa kula chakula chochote, kujumuisha wadudu, minyoo, magamba ya miti, takataka na hata nguruwe wengine. Wakiwa mwituni hula majani, nyasi, mizizi, matunda na maua. Kwa nadra, nguruwe wakiwa wanafugwa, huweza kula watoto wao kama wakichukizwa sana.

Nguruwe wa kawaida wana kichwa kikubwa chenye pua ndefu iliyoimarishwa kwa mfupa mgumu na mduara wa tishu ngumu mbele. Pua hiyo hutumika kuchimba udongo ili kutafuta chakula na ni ogani yenye uwezo mkubwa wa kuhisi.

Nguruwe huwa na seti kubwa ya meno 44. Meno ya nyuma yametoholewa kusaga, na huendelea kukua na huchongwa na misuguano ya meno yenyewe.

Nguruwe wanaochungwa mwituni kwa msaada wa wachungaji, wana uwezo mkubwa wa kunusa, na hutumika kutafuta uyoga katika nchi nyingi za Ulaya.

Nguruwe wa nyumbani hutambulika kwa jina la kisayansi 'Sus scrofa'. Walianza kufugwa karibu miaka 5,000 mpaka 7,000 iliyopita. Walizaliwa na rangi ya kahawia na kuendelea kuwa wa kijivu. Meno chonge ya juu huwa kama ndovu za kipekee zilizopinda nje na kuelekea juu. Urefu wa nguruwe huweza kufikia milimita 900 – 1800 na uzito wa kg 50 – 350.

Nguruwe wana akili na huweza kufundishwa kazi na mbinu ndogondogo. Hivi karibuni, wamefurahia kupewa nafasi kama wanyama kipenzi wa ndani na, hasa wale nguruwe wadogo.

Pia kwa baadhi ya imani za kidini humchukulia nguruwe kama haramu, wakati wengine hufurahia nyama yake na kudai ndiyo nyama yenye ladha maridadi kuliko wanyama wengine.

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nguruwe-kaya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy