Nenda kwa yaliyomo

Athi River

Majiranukta: 01°27′S 36°59′E / 1.450°S 36.983°E / -1.450; 36.983
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hii ni makala juu ya mji wa Athi River. Angalia pia Mto wa Athi-Galana-Sabaki
Mji wa Athi River.

Athi River (inajulikana pia kama Mavoko) ni mji nchini Kenya kando ya jiji la Nairobi[1].

Mji huo ni makao ya Baraza la Mji wa Mavoko na ni mji mkuu wa divisheni ya Mavoko ambayo ni sehemu ya kaunti ya Machakos. Pia ni kata ya kaunti ya Machakos, Eneo bunge la Mavoko[2].

Idadi ya wakazi wa mjini ni 22,000 na jumla ya wakazi ni 139,380 (sensa ya 2009 [3]).

Mji huu umeendelea kiasi, ukiwa pamoja na kiwanda kikubwa cha saruji kinachoendeshwa na kampuni ya Athi River Mining. Mji wa Athi River pia unakua kuwa eneo la makazi kutokana na ukaribu wake na Nairobi.

Uchukuzi

[hariri | hariri chanzo]

Mji huu una kituo cha reli kilicho jengwa mwaka wa 1920 kwenye njia ya reli Mombasa - Nairobi. Chuo Kikuu cha Daystar kina tawi katika mji wa Athi River. Jina la mji huu linatokana na Athi, sehemu ya kwanza ya mfumo wa mto Athi-Galana .

Mji wa Athi River unafuatana na uko kilometa tatu kutoka mji wa Kitengela , lakini ni sehemu ya Wilaya ya Machakos katika Mkoa wa Mashariki, ilhali Kitengela uko kwenye Wilaya ya Kajiado katika Mkoa wa Bonde la Ufa.

Mavoko ilichongwa kutoka kwa Baraza la Mji wa Nairobi mwaka 1963, wakati Baraza hilo lilipofutiliwa mbali. Manisipaa ya Mavoko ina kata sita (Athi River Magharibi, Katani, Kinanie/Mathani, Makadara, Muthwani na Sophia). Zote hizi zimo kwenye eneo bunge la Kathiani, ambayo ina jumla ya wadi kumi. Wadi nne zilizobaki zimo kwenye Baraza ya Mji wa Masaku.

  1. Daily Nation, Aug 21, 2000: Town touched by tragedy
  2. Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency Archived Septemba 29, 2007, at the Wayback Machine
  3. Kenya National Bureau of Statistics: Idadi ya watu wa serikali za mitaa

01°27′S 36°59′E / 1.450°S 36.983°E / -1.450; 36.983

pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy