Nenda kwa yaliyomo

Kaunti ya Marsabit

Majiranukta: 2°19′N 37°58′E / 2.317°N 37.967°E / 2.317; 37.967
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaunti ya Marsabit
Kaunti
Makao Makuu ya serikali ya Kaunti ya Marsabit
Bendera Nembo ya Serikali
Marsabit County in Kenya.svg
Kaunti ya Marsabit katika Kenya
Coordinates: 2°19′N 37°58′E / 2.317°N 37.967°E / 2.317; 37.967
Nchi Kenya
Namba10
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuMarsabit
Miji mingineMoyale, Sololo
GavanaMohsmuf Mohamed Ali
Naibu wa GavanaSolomon Gubo Riwe
SenetaGodana Hargura
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Safia Sheikh Adan
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Marsabit
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa20
Maeneo bunge/Kaunti ndogo4
Eneokm2 70 944.1 (sq mi 27 391.7)
Idadi ya watu459,785
Wiani wa idadi ya watu6
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutimarsabit.go.ke

Kaunti ya Marsabit ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 459,785 katika eneo la km2 70,944.1, msongamano ukiwa hivyo wa watu 6 kwa kilometa mraba[1]..

Makao makuu yako Marsabit. Mji mkubwa zaidi ni Moyale ulio katika mpaka wa Kenya na Uhabeshi.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya marsabit ni kavu. Ina Jangwa la Chalbi ambalo ni jangwa halisi pekee katika Kenya.

Kaunti za Marsabit, Turkana na Samburu hushiriki Ziwa Turkana.

Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi hupatikana katika fuo za Ziwa Turkana upande wa Marsabit. Hifadhi ya Taifa ya Losai hupatikana katika mpaka wa Kaunti ya Marsabit na Samburu. Mlima Marsabit uko katika Hifadhi ya Taifa ya Marsabit. Mlima Kulal na Vilima vya Huri hupatikana katika kaunti hii.

Kaunti ya Marsabit imegawanywa maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bunge Kata
Moyale Butiye, Sololo, Heillu/Manyatta, Golbo, Moyale Mjini, Uran, Obbu
North Horr Dukana, Maikona, Turbi, Horr Kaskazini, Illeret
Saku Sagate/Jaldesa, Karare, Marsabit ya Kati
Laisamis Loiyangalani, Kargi/Horr Kusini, Korr/Ngurunit, Logo Logo, Laisamis

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

[hariri | hariri chanzo]
  • Loiyangalani 35,713
  • Marsabit Central 79,181
  • Marsabit North 54,297
  • Marsabit South 65,376
  • Moyale 108,949
  • North Horr 71,447
  • Sololo 44,822

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.
  2. "Kuhusu Marsabit Ilihifadhiwa 29 Machi 2018 kwenye Wayback Machine.", Serikali ya Marsabit, ilipatikana 13-04-2018
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy