Nenda kwa yaliyomo

Homa ya mafua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtu anaye umwa Homa ya mafua

Homa ya mafua ni ugonjwa wa kuambukiza unaojulikana pia kwa jina lenye asili ya Kiitalia influenza (yaani "athari") na kwa kifupi chake flu. Kwa Kiswahili unaitwa pia kaputula au Homa ya kaptura kwa sababu uliingia Afrika Mashariki pamoja na kaptura.[1]

Dalili zake zinafanana katika mengi na mafua ya kawaida lakini ni kali zaidi. Homa ya mafua inasababishwa na virusi vya influenza aina A au B, mara chache pia aina C.

Homa ya mafua inaathiri kila mwaka asilimia 10 hadi 20 za watu wote duniani.

Dalili za homa ya mafua ni pamoja na kikohozi, maumivu shingoni, maumivu ya misuli, maumivu ya kichwa na homa. Wakati mwingine, lakini si kwa kawaida, kunatokea pia kutapika na kuhara.

Homa ya mafua inaweza kudhoofisha mwili na kufungua hivyo mlango kwa magonjwa mengine kama vile kifua kikuu. Hii ni sababu ya kwamba homa ya mafua inaweza kuwa hatari kwa watoto na wazee hasa na kusababisha ugonjwa mkali hadi kifo.

Ambukizo

[hariri | hariri chanzo]

Virusi vyake vinaingia mwilini kupitia ngozi kamasi za pua, mdomo na jicho. Kwa hiyo vinapitishwa kwa urahisi wakati mgonjwa anakohoa au kupiga chafya. Katika tendo hili matone madogo ya kamasi yenye virusi yanatoka mdomoni au puani na kuelea hewani kwa muda mfupi. Mtu mwingine anayepigwa na matone yale madogo yasiyoonekana kwa macho anaweza kupokea matone kadhaa wakati wa kupumua na kuambukizwa kwa njia hii.

Kuvaa gubizi ya kitambaa juu ya mdomo na pua inapunguza hatari, maana matone mengi yanashikwa na kitambaa wakati wa kukohoa na kinyume mtu asiyeambukizwa analindwa kwa njia hiyo pia.

Kunawa mikono mara kwa mara hupunguza hatari ya maambukizi kwa kuwa virusi hufanywa tuli kwa sabuni.[2] Kuvaa kinyago cha upasuaji pia ni muhimu.[2]

Chanjo ya influenza ya kila mwaka imependekezwa na Shirika la Afya Duniani kwa walio katika hatari sana. Chanjo hii husaidia dhidi ya aina tatu au nne za influenza.[3] Kwa kawaida hustahimilika vyema. Chanjo iliyotengenezwa kwa mwaka mmoja huenda isitumike katika mwaka ufuatao, kwa kuwa virusi hubadilika haraka.

Vitamini D inasaidia kuimarisha kinga asilia ya mwilini dhidi ya maambukizo.

Hakuna tiba ya homa ya mafua isipokuwa kupumzika na kuepukana na kazi zote na kusubiri hadi kinga ya mwili iwe imepambana na virusi. Kuna dawa zinazoweza kupunguza dalili kama homa au maumivu.

Siku hizi kuna pia dawa za antiviral zinazopunguza ukali wa ugonjwa wenyewe bila kuutibu moja kwa moja. Dawa hizo zitumiwe tu baada ya kumwona daktari atakayeamua kama zinafaa au zinaweza kuwa hatari kwa mgonjwa.

Tatizo ni hasa kwamba virusi vya homa ya mafua vinabadilika haraka; hivyo kuna watu wanaoambukizwa influenza upya mwaka baada ya mwaka.

Hali ya hatari inatokea hasahasa kwa sababu influenza ni ugonjwa wa zuonosia. Virusi vya influenza vya ndege au nguruwe vinaweza kuhama kutoka kwa wanyama na kumwathiri binadamu. Kama virusi hivyo vyenye asili ya wanyama vinaweza pia kupitishwa kutoka mtu hadi mtu, vinaingia mwilini kama virusi vipya visivyojulikana bado na mfumo wa kingamaradhi na kusababisha magonjwa mazito ya watu wengi kiasi. Hii inatokea kila baada ya miaka kadhaa na kusababisha vifo.

Dawa za kupambana na virusi kama vile kizuio cha neuraminidase oseltamivir miongoni mwa nyingine zimetumika kutibu influenza.[3] Manufaa yake kwa walio na afya bora hayaonekani kuwa zaidi ya hatari zake.[4] Hakuna manufaa yaliyopatikana kwa wale walio na matatizo mengine ya kiafya.[4][5]

  1. Ndivyo inavyosema kamusi ya Johnson. Zile za baadaye zinahusianisha kaputula na kuharisha.
  2. 2.0 2.1 Jefferson T, Del Mar CB, Dooley L; na wenz. (2011). "Physical interventions to interrupt or reduce the spread of respiratory viruses". Cochrane Database Syst Rev (7): CD006207. doi:10.1002/14651858.CD006207.pub4. PMID 21735402. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. 3.0 3.1 "Influenza (Seasonal) Fact sheet N°211". who.int. Machi 2014. Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 Michiels, B; Van Puyenbroeck, K; Verhoeven, V; Vermeire, E; Coenen, S (2013). "The value of neuraminidase inhibitors for the prevention and treatment of seasonal influenza: a systematic review of systematic reviews". PLoS ONE. 8 (4): e60348. doi:10.1371/journal.pone.0060348. PMC 3614893. PMID 23565231.{{cite journal}}: CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  5. Ebell, MH; Call, M; Shinholser, J (Aprili 2013). "Effectiveness of oseltamivir in adults: a meta-analysis of published and unpublished clinical trials". Family practice. 30 (2): 125–33. doi:10.1093/fampra/cms059. PMID 22997224.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa ya mafua kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
pFad - Phonifier reborn

Pfad - The Proxy pFad of © 2024 Garber Painting. All rights reserved.

Note: This service is not intended for secure transactions such as banking, social media, email, or purchasing. Use at your own risk. We assume no liability whatsoever for broken pages.


Alternative Proxies:

Alternative Proxy

pFad Proxy

pFad v3 Proxy

pFad v4 Proxy